đź“Ś*Dkt. Samia aweka historia kupandisha bei kahawa kutoka 1200 hadi 6,000 kwa kilo*
đź“Ś*Dkt. Biteko ampongeza Rais Samia kwa jitihada zake za kutatua changamoto za zao la kahawa*
*Na Ofisi ya Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati*
Hivi karibuni Bodi ya Kahawa Tanzania (TCB) imesema kuwa imejipanga kushirikiana na wadau nchini ili kuongeza uzalishaji wenye tija wa zao la kahawa kutoka tani 70,000 hadi kufikia 300,000 ifikapo mwaka 2025 kwa kuwa ni zao la kimkakati.
Aidha, sekta binafsi na za umma zinashauriwa kuwekeza katika kuongeza uzalishaji wa zao hilo kutokana na umuhimu wake na fursa zake kiuchumi.
Akizungumza Desemba 19, 2024 katika Uwanja wa Kaitaba wilayani Bukoba mkoani Kagera wakati aliposhiriki Tamasha la Pili la Uwekezaji la mkoa huo ikiwa sehemu ya Wiki ya Tamasha la Ijuka Omuka (Kumbuka Nyumbani), Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko ametoa wito kwa wawekezaji kuwekeza katika mkoa huo kufuatia fursa mbalimbali zilizopo hususan kilimo cha zao la kahawa.
“Mkoa wa Kagera unayo fursa kubwa ya kilimo cha kahawa kutokana na uwepo wa hali nzuri ya hewa na mvua zinazonyesha misimu miwili kwa mwaka. Licha ya kuwa mkoa huu unaongoza kitaifa kwa uzalishaji wa kahawa kwa wastani wa tani 60,000 – 80,000 kwa mwaka, bado kuna fursa ya kuongeza uzalishaji huo hadi kufikia tani 300,000 kwa mwaka kwa kuongeza mashamba ya kahawa,” amesema Dkt. Biteko.
Ameongeza “Nimshukuru Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa jitihada na utendaji kazi wake mzuri, uliowezesha kupanda kwa bei ya kahawa kutoka wastani wa shilingi 1,200 kwa mwaka 2023 hadi wastani wa shilingi 5,000 – 6,000 kwa mwaka 2024 kwa kilo moja ya kahawa ya maganda. Ni rai yangu kwamba, tuendelee kumuunga mkono Mhe. Rais kwa kumaliza changamoto na kupata ufumbuzi ndani ya muda mfupi wa uongozi wake.”
EmoticonEmoticon