Na Mwandishi Maalum , Zanzibar
Chama cha Mapinduzi (CCM) kimesema hakitaacha kushughulika na changamoto zinazowakabilii wananchi kwakuwa hiyo ni moja ya shabaha ya kuanzishwa CCM mwaka 1977.
Kimesisitiza kazi ya kupigania haki za wananchi, uhuru,kuenzi thamani ya utu na heshima ya kila binadamu, majukumu hayo yalianza kutekelezwa na vyama vya TANU na ASP.
Matamshi hayo yametamkwa na Katibu wa Kamati Maalum ya Nec Zanzibar, Idara ya itikadi, Uenezi na Mafunzo ,Khamis Mbeto Khamis, wakati akijibu swali la sababu ipi inayowafanya watanzania kuendelea kuichagua CCM .
Mbeto akijibu swali hilo, alisema watanzania wataendelea kuiamini CCM kutokana na kusimamia malengo ya kuanzishwa kwake, sera na siasa yake pia ni chama kinachoshughilika na matatizo ya wananchi
Alisema CCM haitaacha wala kupuuzia kutafuta majibu yoyote ya matatizo yanayowakabili wananchi katika kila Mtaa, Kkijiji, Kitongoji, Wadi/Kata,Wilaya hadi Mkoa .
"Chama kinachopigania maslahi ya umma hakiwezi kunyimwa kura au kutoaminiwa. Kitaendelea kushinda kwakuwa watanzania wanaiamini na kuitegemea CCM kwa kutumikia kwake wananchi "Alisema mbeto
Aidha alisema chama kinachohangaikia shida na matatizo ya watu , kinachotafuta majibu ya matatizo na kuwafikia wananchi ,kuwasikiliza na kutoa ufumbuzi, lazima kiaminiwe na kushinda .
'Nadhani upinzani ubadilishe mtindo wa siasa zake ili ukubalike katika jamii. Kubeza au kupondoka kila jema la CCM si mtaji utakaoufanya upinzami uungwe mkono. Kwa mtindo huo itawachukua miaka mia moja ijayo hadi uaminike" Alieleza
Pia alivishauri vyama hivyo kuungana na kuunda chama kimoja kitakachokuwa na nguvu za ushindani kwa CCM, kwani kadri unavyooendelea kubaki na utitiri wa vyama, hautakishanda chama tawala.
"kazi ya kushughulika na mataizo ya wananchi hicho ni kiapo kwetu. Ni jukumu la kufa na kupona .Kinachotuumiza kichwa CCM usiku na mchana ni kupata maendeleo ya nchi na watu"Alieleza Mbeto
EmoticonEmoticon