SOLO MNAMUNGA AIBUKA KIDEDEA UCHAGUZI KOROGWE VIJIJINI CHADEMA

November 14, 2024


NA MWANDISHI WETU,Korogwe

KADA wa siku nyingi wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Oliva Kisaka maarufu Solo Mnamunga sasa ni Mwenyekiti mpya wa chama hicho Korogwe Vijijini mkoani Tanga baada ya kupata ushindi wa kishindo dhidi ya mpinzani wake wa karibu, Salim Sempoli.

Uchaguzi huo kwa mujibu wa Katiba ya Chadema ulifanyika mwishoni mwa wiki iliyopita, na Solo alipata kura 53 huku mpinzani wake, Sempoli akiambulia kura 33 kati ya kura 86 zilizopigwa na wajumbe kutoka kata zote 29 za Jimbo la Korogwe Vijijini.

Mbali na mwenyekiti, nafasi zingine mbalimbali zilishindaniwa na kupata washindi ambao wanatarajiwa kukisaidia chama hicho kuendelea kujitanua na kuleta ushindani mkubwa wa kisiasa dhidi ya Chama Cha Mapindizi (CCM).

Washindi waliotangazwa kwenye mkutano huo ni pamoja na Mwenyekiti, Oliva Kisaka (Solo), Katibu, Thomas Lwoga aliyepata kura 48 dhidi ya Lucyana Andrea aliyeambulia kura 39.

Aidha nafasi zingine ni kama ifuatavyo kwenye mabano, Katibu Mwenezi (Ibrahim Wiss), mweka hazina (Twaha Juma), Mjumbe wa mkutano mkuu (Jumanne Billa), Mjumbe (Ramadhani Kihiyo), Baraza la Wazee, mtunza hazina ni (Said Ally Daffa), naibu katibu (Athuman Ndiga), katibu ni (Ally Juma Mtangi).

wengine ni makamu mwenyekiti (Jalali Salehe Mjenga), Mwenyekiti (Josiah Tumaini) huku nafasi katika Baraza la wanawake za wanawake (BAWACHA) washindi wakiwa ni Aminata Saguti (mwenyekiti),  katibu (Mwajuma Abdalla), mratibu wa uenezi akitajwa kuwa ni Anjelina Mhina na mweka hazina ni Esta Dastan. Kwa upande wa Bavicha, Mwenyekiti ni George Shafi, katibu ni Kaimu Yahaya, katibu mwenenzi ni Msumari Kembo na mweka hazina akiwa ni Adinan Hamisi huku mjmbe wa kaati ya utendaji akiwa ni Rehema Idd.


Share this

Related Posts

Previous
Next Post »