Akizungumza katika uzinduzi huo Ans. Makola kutoka dawati la Jinsia na watoto Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam ameipongeza People Development Forum (PDF) na Jenga hub kwa kutoa mafunzo hayo kwa watoto na kutoa Wito kwa wazazi, Walezi na Walimu kuchukua tahadhari na kumwelekeza mtoto jinsi ya kutumia mitandao abaki salama bila kufanyiwa ukatili kwani ni vigumu kumnyima mtoto kutumia Mtandao katika Zama hizi za Kidigitali.
"Mradi huu ni hatua muhimu ya kuwalinda watoto wetu na kuwawezesha kuelewa jinsi ya kujilinda. Tunawapongeza PDF na wadau wake kwa dhamira yenu ya kujenga mazingira salama ya mtandaoni kwa watoto wetu.
"Ikumbukwe kuwa hatua hizi ni baada ya Serikali kupitia wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu kuzindua kampeni ya ulinzi na usalama wa mtoto Mtandaoni mnamo Mnamo tarehe 11/02/2024 dhima ikiwa ni kuendelea kukabiliana na Ulimwengu wa kidigitali ili kupunguza matukio ya ukaliti mtandaoni ambayo ilienda sambamba na kauli mbiu isemayo “Ni Jukumu Letu; Chukua hatua”Waziri wa wizara hiyo Dkt. Doroth Gwajima aliweka bayana utafiti uolifanywa na Serikali kwa kushirikiana na Shirika la UNICEF mwaka 2022 kuwa watoto 4 tayari ni wahanga wa ukatili huo na kuweka mikakati madhubuti ya Wizara kwa kushirikiana na wadau, mashirika ya kiserikali na yasiyo ya kiserikali kumuelimisha Mtoto, kuanzishwa kwa madawati ya ulinzi na usalama wa watoto ndani na nje ya shule pamoja na kumuelimisha Mzazi juu ya matumizi sahihi ya mtandao kwa mtoto.
“Utafiti uliofanywa na Serikali kwa kushirikiana na Shirika la UNICEF mwaka 2022 kwa watoto wa Tanzania wa umri wa miaka 12 hadi 17 ulionesha asilimia 67 ya watoto wanatumia mitandao na asilimia 4 ya watoto hao walifanyiwa ukatili kwenye mitandao” Dkt. Gwajima.
Nao wanufaika wa Mradi huo ambao ni watoto wameahidi kufanyia kazi mafunzo waliyoyapata ikiwa ni pamoja na kutoa elimu kwa wote jinsi ya kutumia mitandao kwa manufaa hasa katika masomo yao.
EmoticonEmoticon