KATIBU MKUU WA NLD DOYO AITAKA TAKUKURU KUWA MAKINI NA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA

November 05, 2024

 



Na Paskal Mbunga,Tanga

KATIBU wa Chama cha NLD Taifa Doyo Hassani Doyo ameiomba Taasisi ya kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini (Takukuru) kuwa makini na uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwenye suala la fomu za wagombea kujitoa kutokana na kwamba kanuni hiyo inakwenda kurasimisha rushwa.

 

Doyo aliyasema hayo wakati akizungumza na vyombo vya habari Jijini Tanga kuelekea kwenye uchaguzi huo ambapo alisema kwa kutengeneza fomu hizo za wagombea kujitoa kwanini kanuni iwe na mawazo ya watu kujitoa.

 

Alisema kwa sababu watu wamechukua fomu na akili zao wenyewe timamu na hawajashawishiwa na mtu halafu kuwe na fomu ya kujitoa kugombea nafasi hiyo kwanini hivyo wanaiomba walisimamie zoezi la fomu za kujitoa ili kusiwe na watu waliojitoa.

 

“Tunaomba uchaguzi huu Takukuru waingie kwa kiwango kikubwa kuzuia rushwa hii maana mtu anachukua fomu mwenyewe kwa akili yake timamu bila kushawishi na mtu kujaza fomu ya kugombea nafasi hiyo,kwanini  wajitoa “Alisema

 

Hata hivyo Katibu Doyo aliitaka Wizara ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) kuhakikisha wasimamizi wasaidizi wanakuwa waadilifu kwa fomu ambazo wamechukua wagombea na kuzirejesha.

 

Alisema wawe kwa wagombea waliopitisha basi wawateue bila vikwazo ili waingie ulingoni na kuondoa manung’uniko yaliyojitokeza mwaka 2019 katika utawala uliopita.

 

Alisema kwa sababu tarehe 1 wagombea wamejesha fomu na wamekaa nazo wiki nzima hivyo ni muhumu watumie uadilifu kuona njia nzuri ya kuwateua wagombea ambao wametia nia ya kugombea nafasi mbalimbali kwenye uchaguzi huo bila kuwekewa

 

Hata hivyo alisema kwamba chama hicho hivi sasa wamejipanga imara kuhakikisha kwenye uchaguzi mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani wanasimamisha wagombea makini.

 

Alisema watafanya hivyo wakiwa na nia ya kuhakikisha wanawapa maendeleo watanzania na kuinua uchumi wao katika nyanja mbalimbali.


Share this

Related Posts

Previous
Next Post »