BILIONI 900 KUKARABATI MIUNDOMBINU YA BARABARA NA MADARAJA-TANROADS

September 27, 2024

 


Wakala ya Barabara Tanzania (TANROADS), imetenga zaidi ya shilingi bilioni 900 kwa mwaka wa fedha 2023/2024 kwa ajili ya kukarabati miundombinu ya barabara iliyoharibiwa na mvua za El-Nino na kimbunga Hidaya.

Hayo yamesemwa leo jijini Dar es Salaam na Kaimu Mtendaji Mkuu wa TANROADS, Ephatar Mlavi, wakati wa mkutano na Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), ambao unaratibiwa na  na Ofisi ya Msajili wa Hazina katika Taasisi zilizochini ya Ofisi hiyo  kuelezea mafanikio ya serikali ya awamu ya sita chini ya uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kuelezea ili wananchi wajue utendaji wa Taasisi hizo.

Amesema ukarabati huo ni juhudi za serikali kuhakikisha miundombinu muhimu ya usafirishaji inabaki katika kuwa imara katika kutoa huduma kwa  wananchi kuendelea kuzalisha na uchumi kuendelea kukua.

Mlavi, TANROADS inasimamia mtandao wa barabara wenye urefu wa zaidi ya kilometa 37,000 kote nchini, ikiwa ni pamoja na ujenzi, ukarabati, na matengenezo ya barabara na madaraja na jukumu lingine ni ujenzi wa viwanja vya ndege.

Amesema katika kufanya majukumu hayo kunaongeza  ufanisi wa miundombinu ya usafirishaji na kuchangia  maendeleo ya kijamii na kiuchumi nchini.

Mlavi amesema kuwa Tanroads imepewa kazi katika imepewa fedha kwa ajili  ya kufunga  taa za barabarani, ambazo zinalenga kuboresha usalama wa barabarani pamoja kunawirisha  mandhari ya miji nchini

Amesema hatua hiyib inatarajiwa kuongeza usalama wa watumiaji wa barabara hasa wakati wa usiku na kupunguza ajali zinazoweza kutokea kutokana na giza.

Amesema ujenzi wa daraja la Jangwani, linalounganisha Magomeni Mapipa na Fire ipo katika mipango ya  serikali  katika hatua za mwisho za kusaini mkataba na mkandarasi, na ambao  unatarajiwa kusainiwa Oktoba mwaka huu

Hata hivyo amesema Daraja hilo ni miradi ya kimkakati inayolenga kupunguza msongamano wa magari na kuimarisha mawasiliano kati ya maeneo muhimu ya jiji la Dar es Salaam.

Mlavi amesema kuwa changamoto wanazokutana nazo wakandarasi wazawa kukosa mitaji mikubwa  ya  kazi kubwa za ujenzi.

Hata hivyo, alifafanua kuwa wakandarasi wa ndani wanachangia takriban asilimia 31.60 ya miradi inayosimamiwa na TANROADS, ikiwa ni ishara ya mchango wao katika maendeleo ya miundombinu ya nchi.

Serikali inaendelea kuhamasisha ushiriki wa wakandarasi hawa kwa kuwajengea uwezo wa kifedha na kitaalamu ili waweze kushindana kwenye miradi mikubwa zaidi.Kaimu Mtendaji Mkuu wa TANROADS, Ephatar Mlavi akizungumza wakati wa mkutano na Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), uliofanyika Jijini Dar es Salaam. chini ya uratibu wa Ofisi ya Msajili wa HazinaKaimu Mkuu wa kitengo cha  Mwasiliano Serikalini Wakala ya  Barabara  Tanzania (TANROADS) Aisha Malima akizungumza katika kikao hicho.Afisa Habari Ofisi ya Majili wa Hazina ,Alex Malanga akizungumza alipokuwa akitoa salamu za utangulizi katika kikao kazi hicho.


Baadhi ya wahariri wakiuliza maswali baada ya kutolewa kwa taarifa ya Tanroads katika kikao kinachoratibiwa na Ofisi ya Msajili jijini Dar es Salaam.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »