Na Oscar Assenga,TANGA
KAMATI ya Bunge Uwekezaji na Mitaji ya Umma (PIC) imeridhishwa na miradi inayotekelezwa na Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira (Tanga Uwasa) huku wakizitaka mamlaka nyengine nchini kwenda kujifunza ubunifu ambao wanautumia katika kutekeleza miradi yao na hivyo kuwawezesha kuondoa changamoto hiyo kwa wananchi.
Hayo yalisemwa juzi na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu
ya Bunge Uwekezaji wa Mitaji ya Umma Deus Sangu wakati wa ziara ya kutembelea
na kukagua miradi inayotekelezwa na Tanga Uwasa ambapo wameridhishwa na miradi
hiyo huku akiipongeza Serikali kwa namna
inavyopeleka msukumo kwenye uwekezaji hasa kwenye sekta ya ya maji .
Alisema kamati hiyo imejionea shuguli uwekezaji na
kuona ubunifu kamati imekagua mradi huo imerdhishwa na ubunifu huo huku
kuwataka mamlaka nyengine ziweze kuiga mfano wa kuona namna ya kutatua
changamoto ya maji katika maeneo yao.
“Mradi huu umetekelezwa kwa mkopo kutoka benki ya
maendeleo asilimia 75 na sehemu inayobakia
kama bilioni 3 ni makusanyo ya ndani hivyo mradi huu zaidi ya Bilioni 10 na umeleta mapinduzi makubwa
sana kwa maana mahitaji ya maji jiji la
Tanga lita milioni 45,000,000 “alisema
Aidha alisema wao kama kamati wameridhishwa na namna
ambavyo Tanga Uwasa walivyoweza kubuni vyanzo vya kufadhili miradi yao na wameona
mamlaka za maji wanategemea vyanzo kutoka serikali kuu lakini wao wenyewe
wamebuni na kwenda kukopa fedha benki na mapato yao ya ndani wakaleta mapinduzi
na kutatua changamoto ya maji karibunia
takribinia asilimia 96.
Alisema pia kwanza
kuja na hati fungani wamekuja na ubunifu wa kipekee kwa taaswanza Tanzania kuja
na hati fungani ya kijani yenye thamani ya bilioni 53 itakayosaidia kuongeza
kiwango cha maji kwa kiasi kikubwa huo mradi kwa kikasi kikubwa ilikuwa iongeze
hiy ni heshima ya kipekee kwa Tanga Uwasa kuanzisha kwa jambo hilo.
“Sisi kama tunawapongeza na kuzitaka mamlaka za maji
kuona namna kujifunza Tanga uwasa kwa jinsi wanavyofanya a Tanga Uwasa
walivyotumia mapato yake ya ndani kuweza kwa kutekeleza miradi yake na kuwa na
tija kubwa”Alisema
Awali akkizungumza Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya
Tanga Uwasa Dkt Ally Fungo aliishukuru hiyo kwa kuwapa ushauri na maelekezo na
ushauri wao ndio wameweza kufika hapo hiyo ni sehemu ya awamu ya awali ya mradi
ambao baada ya kuchukua mkopo wa awali wa shilling zaidi ya bilioni 7.
Alisema hivyo walikuwa wanajenga uhalali na uzoefu wa kuchukua mkopo mkubwa zaidi na wanataraji kuanzia mwezi wa nne mwaka huu
wataanza kutekeleza miradi mingine zaidi ili kufikia lita milioni 60 na kufikia
wananchi wote wa Tanga,Pangani,Muheza,Pangani na Mkinga.
“Hivyo niwashukuru bodi kuhakikisha tunakuja na mipango mizuri ya kuhakikisha hkila siku hawalali na kuhakikisha wanakuja na mipango mipaya kuhakikisha wananchi waondokana na gharama za kugharamia huduma mbalimbali”alisema
EmoticonEmoticon