SHABIKI WA YANGA ASHINDA SHILINGI MILIONI 120.1 ZA M-BET

September 12, 2023

 

 Mkurugenzi wa Masoko wa  kampuni ya M-BET Tanzania, Allen Mushi (kulia) akimkabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya Sh120,989,610 shabiki wa Yanga, Paulo Martin baada ya kubashiri kwa usahihi matokeo ya mechi 12 ka droo ya  Perfect 12 y kampuni ya M-Bet.

Shabiki wa klabu ya Yanga, Paulo Martin akipozi baada ya kukabidhiwa mfano wa hundi yenye thamani ya Sh120,989,610 baada ya kubashiri kwa usahihi matokeo ya mechi 12 ka droo ya  Perfect 12 y kampuni ya M-Bet.

…………………….. 

Na Mwandishi wetu

- Advertisement -
Ad image

Dar es Salaam. Shabiki wa klabu ya Yanga wa, Paulo  Martin ameshinda  Sh120,989,610 baada ya kubashiri kwa usahihi mechi 12 za ligi mbalimbali duniani kupitia mchezo wa Perfect 12 wa kampuni ya M-Bet.

Martin ambaye ni mwanajeshi wa Jeshi na mjasiriamali alikabidhiwa fedha zake na Mkurugenzi wa Masoko wa  M-Bet Tanzania, Allen Mushi katika hafla fupi iliyofanyika jana jijini Dar es Salaam.

Mushi alisema kuwa Martin anaungana na washindi wengine mbalimbali ambao wameshinda mamilioni kupitia droo ya Perfect 12 na kuweza kubadilisha maisha yao.

“Martin anakuwa mmoja wa wanachama wa nyumba yao ya mabingwa ambao kwa sasa imesheheni mamilionea mbalimbali. Tunaposema M-Bet ni nyumba ya mabingwa tunakuwa na maana maalum, mpaka sasa tumewazadia mamilioni washindi mbalimbali” alisema Mushi.

Alisema kuwa M-Bet itaendelea kubadilisha maisha ya Watanzania kupitia michezo yake mbalimbali ya kubashiri na kuwaomba watu wenye umri kuanzia miaka 18 kushiriki.

“Kubashiri si kazi, naomba watu wajue, ni burudani ambayo inakufanya kuibuka milionea endapo utashinda.M-Bet inajisikia fahari sana kuendelea kuwatoa washindi na kubadili maisha yao,” alisisitiza Mushi.

Kwa upande wake, Martin alisema kuwa alianza kubashiri miaka mitatu iliyopita na anashukuru ndoto zake kutimia.

“Nimeanza kubashiri kupitia M-Bet na sijahama kwa sababu ni kampuni imekuwa ikitangaza washindi wengi. Nimeona washindi wengi na nikaamini kuwa ipo siku na mimi nitakuwa natangazwa kwa ushindi. Ndoto yangu imetimia. Nitatumia fedha hizo kwa kuendelea biashara zangu na shughuli nyingine za kimaendeleo,” alisema Paulo.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »