WAZIRI LUKUVI ARIDHISHWA NA MAANDALIZI YA MAADHIMISHO YA SIKU YA MASHUJAA 2025

July 16, 2025


Na Mwandishi wetu- DODOMA


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), Mhe. William Lukuvi amefanya ukaguzi wa maandalizi ya Maadhimisho ya Siku ya Mashujaa yanayotarajiwa kufanyika tarehe  25 Julai 2025 katika Uwanja wa Mashujaa, Mtumba – Dodoma.

Maadhimisho hayo yatapambwa na gwaride kutoka *majeshi matano ya ulinzi na usalama* na mgeni rasmi atakuwa *Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania*, Mhe. *Dkt. Samia Suluhu Hassan*.

Katika ziara hiyo, iliyofanyika leo tarehe 16 Julai, 2025 jijini Dodoma Waziri Lukuvi aliambatana na viongozi waandamizi kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu pamoja na maafisa kutoka JWTZ na Jeshi la Polisi.


Maandalizi yameelezwa kuendelea vizuri, huku tukio hilo likitarajiwa kuwa la Kitaifa  na kihistoria katika kutoa heshima kwa mashujaa wa Tanzania.



MWISHO

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »