Meza kuu wakifuatilia matukio mbalimbali katika maadhimiosho hayo
Katibu wa Tana Tawi Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga Mwanaisha Nyangasa akisoma risala |
Kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga Bombo Dkt Juma Ramadhani akizungumza wakati alipotembelea mabanda mbalimbali |
Kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga Bombo Dkt Juma Ramadhani kulia akigawa zawadi kwa mgonjwa aliyelazwa kwenye Hospitali hiyo ikiwa ni maadhimisho ya siku ya wauguzu Duniani |
Muuguzi Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga Bombo Andrew Tusiwe akigawa zawadi kwa wagonjwa katika hospitali hiyo |
Maandamano ya wauguzi kutoka Kituo cha Toyota kuelekea Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga Bombo ikiwa ni kuadhimisha siku ya wauguzi duniani
Wauguzi wakiwa kwenye maandamano hayo
Wauguzi wakianza maandamano ikiwa ni siku ya maadhimisho ya siku ya wauguzi Duniani
Mkuu wa Idara ya Tehama katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga Bombo William Masika akicheza wakati wa maandamano hayo ya siku ya wauguzi duniani yalipopokelewa |
Mkuu wa Idara ya Tehama katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga Bombo William Masika akicheza wakati wa maandamano hayo ya siku ya wauguzi duniani yalipopokelewa |
Sehemu ya wauguzi katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga Bombo wakifuatilia matukio mbalimbali wakati wa maadhimisho hayo |
Na Oscar Assenga,TANGA
KAIMU Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga Bombo Dkt Juma Ramadhani leo amewaongoza wauguzi katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa kwenye maaadhimisho ya siku ya Wauguzi Duniani ambapo kilele chake kitafanyika Mei 12 Jijini Mwanzasiku ya wauguzi Duniani.
Maadhimisho hayo yalianza na maandamano kutoka eneo la Toyota mpaka Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga Bombo kulipofanyika kilele cha maadhimisho hayo
Akizungumza wakati wa maadhimisho hayo,Dkt Juma alisema kutokana na uwepo wa changamoto ya usafiri kwenye mkoa huo ambayo ilielezwa wakati wa risala ya wauguzi hao alieleza mipango ya uongozi wa hospitali hiyo kwenye bajeti zijazo na jitihada walizoweka kama taasisi wana mpango wa kununua basi ili kupunguza adha ya usafiri kwa watumishi.
Dkt Juma alisema basi hilo kwa ajili ya Hospitali hiyo ambalo linaweza kupunguza changamoto ya uchelewaji kazini kutokana na hali hiyo na kwamba tayari wameshaliona na wameliweka kwenye mpango wao kuweza kulitatua
“Hili la changamoto ya kuchelewa kazini kutokana na changamoto ya usafiri kwenye mkoa wetu hilo tumeliona kama uongozi wa Hospitali kwenye bajeti zijazo na jitihada tulizowekeza taasisi wana mpango wa kununua basi kwa ajili ya hospitali ambalo linaweza kupunguza changamoto ya uchelewaji kazini “Alisema Kaimu Mganga Mfawidhi Dkt Juma.
Awali akisoma risala hiyo Katibu wa Tana Tawi Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga Mwanaisha Nyangasa alisema maadhimisho hayo ni kutafakari na kufauta nyayo za mwanzilishi wa huduma za uuguzi na ukunga Bi Florence Night Ngare.
Alisema wauguzi katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga Bombo wamemuenzi kwa kutoa huduma mbalimbali wakati wa maadhimisho hayo ikiwemo za uchunguzi wa saratani ya kizazi na matiti kwa wakina mama ,uchunguzi wa kisukari na macho,shinikizo la damu,kuhamasisha uchangia damu ,upimaji wa VVU kwa hiari na sambamba na utoaji elimu ya afya na lishe kwa wateja mbalimbali
Aidha alisema pia katika maadhimisho hayo wametoa chanjo za Covid 19 ambapo wananchi waliohudumiwa tokea walipoanza maadhimisho hayo ni 154 ambao walihudumiwa kwa siku moja.
Hata hivyo alisema kwamba Ukunga ni kada muhimu sana katika kufanikisha utoaji wa huduma nzuri za afya kwenye jamii na unapozungumzia afya bora muuguzi ni sehemu sahihi ya kufanikisha kila mtanzania anakuwa na afya bora.
Alisema kwamba pamoja hayo kuna mafanikio makubwa ikiwemo mazingira ya kufanyia kazi yameboresha na miundombinu ya hospital na kuwezesha wanafanyakazi kufanya kazi kwenye mazingira mazuri.
Aidha alisema kwamba pia ni wauguzi kupata nafasi ya kujiendeleza kimasomo,wauguzi kupata motisha mbalimbali,kuongezeka kwa hamasa kwa wauguzi .
Akizungumzia changamoto wanazokabiliana nayo alisema kwamba changamoto kubwa ni upungufu wa watumishi idara ya ukunga na uuguzi kulingana na mahitaji ya jamii kutokana na kuongezeka kwa vitengo na idara ambazo wauguzi wanahitajika.
Alisema pia changamoto nyengine ni kuchelewa kufika kazini kwa watumishi kutokana na kuwepo kwa changamoto ya usafiri kwenye mkoa wa Tanga hivyo upo umuhimu wa uwepo wa usafiri.
Mwisho.
EmoticonEmoticon