Kaimu Meneja wa Bandari ya Tanga Peter Milanzi akizungumza wakati wa ziara hiyo kushoto ni Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Atupele Mwakibete |
Na Oscar Assenga, TANGA.
MATUNDA
ya uwekezaji katika Bandari ya Tanga yameanza kuonekana baada ya Naibu Waziri
wa Ujenzi na Uchukuzi Atupele Mwakibete kueleza kwamba Bandari nhiyo imefanikiwa
kukusanya mapato ya Sh.Bilioni 5 kwa kipindi cha mwezi Januari hadi Machi mwaka
huu
Mwakibete
aliyasema hayo wakati wa ziara yake ya siku moja kutembelea Bandari hiyo ambapo
alisema kwamba mapato hayo yametokana na kukamilika kwa Gati hatua ambayo
imesaidia kuongezeka Kwa shehena ya meli za mizigo.
Alisema kwamba hayo ndio mafanikio yaliyotokana
na uwekezaji wa Takribani na Sh.Bilioni 429 uliofanywa na Serikali katika Bandari
ya Tanga ambao umewezesha kuongezeka kwa shehena ya mizigo hatua ambayo
imepeleka kuongezeka kiasi cha mapato hayo.
“Hii ni kazi nzuri ya uwekezaji ambao umefanywa na Serikali hatua
ambayo imeleta manufaa makubwa katika Bandari ya Tanga hivyo nitoe wito kwa
wafanyabiashara kuitumia Bandari ya Tanga kutokana na kuwa na uweke
Katika hatua
nyengine,Naibu Waziri huyo alitoa muda wa mwezi mmoja kwa shirika la Reli
Tanzani (TRC) kuhakikisha wanajenga miundombinu ya reli katika bandari ya Tanga
ili kurahisha huduma za usafirishaji wa mizigo inayoshushwa kwenye bandari hiyo
kuelekea maeneo mbali mbali ya nchi.
Awali akizungumza Kaimu Meneja wa Bandari ya Tanga
Peter Milanzi alisema ndani ya kipindi Cha miezi mitatu wamepokea Meli kubwa
tano ambazo zimebeba zaidi ya shehena ya mizigo Tani 130,000 .
Hata hivyo alisema kutokana na uingiaji wa Meli
kubwa umesaidia kuwezesha ajira za muda mfupi 100 zimeweza kupatikana .
Mwisho.
EmoticonEmoticon