Na John Mapepele
Waziri
wa Utamaduni, Sanaa na Michezo na Mbunge wa Jimbo la Rufiji. Mhe,
Mohamed Omary Mchengerwa ametoa vifaa vya michezo kwa shule zote za
msingi na Sekondari na wanafunzi wanamichezo wote wanaoshiriki kwenye
mashindano ya michezo kwa shule za Msingi (UMITASHUMTA) na Mashindano
ya Shule za Sekondari (UMISSETA) kwa mwaka 2022 Wilaya ya Rufiji.
Mhe.
Mchengerwa amekabidhi vifaa hivyo kwa Mkuu wa Wilaya ya Rufiji Julai
17, 2022 kwenye shule ya Sekondari ya Ikwiriri Wilaya ya Rufiji
ambapo amesema ameamua kufadhili vifaa hivyo katika Wilaya ya Rufiji
ili kuiendeleza michezo kwa kuwa michezo ni biashara na ajira kubwa
kwa vijana.
“Nimeamua
kusaidia vifaa hivi kwakuwa natambua kwa sasa michezo ni miongoni mwa
chanzo cha ajira na biashara kubwa duniani hivyo ni vema kufanya michezo
kwa umakini mkubwa ili kujipatia ajira” amefafanua
Amewataka wachezaji hao kuwa na nidhamu na kujituma kwa kufanya mazoezi ili waweze kushinda kwenye mashindano mbalimbali.
“Nendeni
mkajitume, michezo ni ajira na furaha wasikilizeni walimu wenu, hata
shuleni mtafanya vizuri”amesisitiza Mhe. Mchengerwa.
Aidha
amesema dhamila ya Serikali kwa sasa ni kuendeleza michezo ambapo
amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mhe, Samia Suluhu
Hassan kwa jitihada kubwa anazofanya kwenye michezo katika kipindi
kifupi cha utawala wake ambazo zimeleta mapinduzi makubwa kwenye sekta
hiyo.
Vifaa hivyo vimegharimu zaidi ya milioni 23 ambazo zimenunua zaidi ya jezi seti 200, trakisuti pea 100, kofia 200 na mipira 100.
Pia
amefadhili Ligi ya mpira wa miguu ya sensa katika Wilaya ya Rufiji
ambapo ametoa seti 6 za jezi kwa timu sita na mipira 12 kwa ajili ya
mashindano hayo.
Amesema
lengo la mashindano hayo ni kuhamasisha wananchi kushiriki
kuhesabiwa kwenye sensa ya kitaifa yam waka huu kwa manufaa mapana ya
wananchi wa Rufiji na Taifa kwa ujumla.
Aidha,
amewahimiza wananchi wa Wilaya ya Rufiji na watanzania wote kujitokeza
kwa wingi Agosti 23, mwaka huu kuhesabiwa kwenye zoezi la sensa kitaifa.
Mwenyekiti
wa Halimashauri ya Wilaya ya Rufiji amemshukuru Mhe. Mchengerwa kwa
jitihada zake na mchango wake kwenye sekta ya michezo ambapo
amemhakikishia kuwa michango anayotoa itatumika vizuri ili kupata
matokeo chanya.
EmoticonEmoticon