Na John Mapepele, Birmingham
Waziri
wa Utamaduni, Sanaa na Michezo. Mhe Mohamed Mchengerwa ameitembelea
timu ya wachezaji wa Tanzania inayoshiriki mashindano ya Jumuiya ya
Madola Birmingham nchini Uingereza na kuitaka kupambana kufa na kupona
ili kurejea na medali.
Mhe.
Mchengerwa ameyasema haya leo Julai 27, 2022 kwenye kambi ya timu hiyo
huku akisisitiza kuwa watanzania wakiongozwa na Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania. Mhe Samia Suluhu Hassan wana matumaini makubwa na
timu hiyo hivyo hawana budi kulinda heshima kubwa waliyopewa na taifa
kwa ujumla.
"Nawaomba
tangulizeni uzalendo ili tuweze kushinda, hii ni vita tunahitaji
kupambana bila kujali idadi yetu wala kitu chochote. Tutashinda."
Amesisitiza Mhe. Mchengerwa
Aidha,
amesema dhamira ya Serikali kwa sasa ni kuinua na kuendeleza michezo
kwa kuwa michezo ni chanzo. Ha ajira na uchumi kwa taifa
"
kwa kutambua hilo ndiyo maana kwa mara ya kwanza Serikali imeamua
kutoa fedha nyingi kwa wachezaji watakaopata medali za dhahabu dola za
kimarekani 10,000, shaba 7500 na fedha 5000 bado zawadi za jumla"
amesisitiza Mhe. Mchengerwa.
Pia
ametumia tukio hilo kutoa pongezi kwa timu ya wanaume na wanawake ya
KABBADI kwa kufuzu kuingia kwenye mashindano ya kombe la Dunia
yatakayofanyika Oktoba mwaka huu nchini India.
Mhe
Mchengerwa ameongozana na Mhe. Musa Sima Mjumbe wa Kamati ya Bunge
inayosimamia wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo na ndugu Saidi Yakubu
Naibu Katibu Mkuu.
EmoticonEmoticon