Kutoka
kushoto ni Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi anayeshughulikia Uvuvi
Dkt. Rashid Tamatamah, Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Uvuvi Tanzania
(TAFIRI) Dkt. Ishmael Kimirei, Mratibu wa Usimamizi Shirikishi wa
Rasilimali za Uvuvi Kusini Magharibi mwa Bahari ya Hindi (SWIOFish) Dkt Nichrous Mlalila na Kaimu Meneja wa Kitengo cha Hifadhi za Bahari na
Maeneo Tengefu (MPRU) Bw. John Komakoma wakiwa kwenye mazungumzo na
Mratibu wa Shirika la Maendeleo la Ujerumani (GIZ) nchini Tanzania Bw.
Ralf Senzel na Mkuu wa Ushirikiano wa Maendeleo kutoka Ubalozi wa
Ujerumani hapa nchini Dkt. Katrin Bornemann waliofika katika ofisi ndogo
za Wizara ya Mifugo na Uvuvi zilizopo jijini Dar es Salaam kwa ajili ya
mazungumzo namna ya kukazia ushirikiano baina ya Tanzania na Ujerumani,
kupitia mradi wa uhifadhi wa bainuai za Bahari ya Hindi na Maeneo
Tengefu ya Ukanda wa Pwani, utakaofadhiliwa na Serikali ya Ujerumani.
(Picha na Edward Kondela – Afisa habari, Wizara ya Mifugo na Uvuvi)
Katibu
Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi anayeshughulikia Uvuvi Dkt. Rashid
Tamatamah akisoma moja ya nyaraka za mradi wa uhifadhi wa bainuai za
Bahari ya Hindi na Maeneo Tengefu ya Ukanda wa Pwani, utakaofadhiliwa na
Serikali ya Ujerumani kuanzia Mwezi Agosti Mwaka huu katika kipindi cha
miaka minne kwa thamani ya Euro Milioni 2.17 sawa na Shilingi za
Kitanzania Bilioni 5.2, mradi utakaotekelezwa Kaskazini mwa Tanzania
katika Wilaya ya Mkinga Mkoani Tanga na Kwale Mkoani Kenya, mara baada
ya kutembelewa na ujumbe kutoka Ubalozi wa Ujerumani hapa nchini na
Shirika la Maendeleo la Ujerumani (GIZ), katika ofisi ndogo za Wizara ya
Mifugo na Uvuvi zilizopo jijini Dar es Salaam, ambapo Dkt. Tamatamah
amesema mradi huo una faida kubwa katika kuhifadhi bainuai na kutoa
elimu kwa jamii inayokaa katika maeneo hayo. (Picha na Edward Kondela –
Afisa habari, Wizara ya Mifugo na Uvuvi)
Mkurugenzi
Mkuu wa Taasisi ya Uvuvi Tanzania (TAFIRI) Dkt. Ishmael Kimirei
akichangia hoja wakati wa mazungumzo baina ya ujumbe wa Tanzania kutoka
Wizara ya Mifugo na Uvuvi na Ubalozi wa Ujerumani hapa nchini pamoja na
Shirika la Maendeleo la Ujerumani (GIZ) juu ya mradi wa uhifadhi wa
bainuai za Bahari ya Hindi na Maeneo Tengefu ya Ukanda wa Pwani,
utakaofadhiliwa na Serikali ya Ujerumani kuanzia Mwezi Agosti mwaka huu.
Mazungumzo hayo yamefanyika katika ofisi ndogo za Wizara ya Mifugo na
Uvuvi zilizopo jijini Dar es Salaam. (Picha na Edward Kondela – Afisa
habari, Wizara ya Mifugo na Uvuvi)
Kutoka
kushoto ni Mratibu wa Usimamizi Shirikishi wa Rasilimali za Uvuvi
Kusini Magharibi mwa Bahari ya Hindi (SWIOFish) Dkt. Nichrous Mlalila na
Kaimu Meneja wa Kitengo cha Hifadhi za Bahari na Maeneo Tengefu (MPRU)
Bw. John Komakoma wakimsikiliza Mratibu wa Shirika la Maendeleo la
Ujerumani (GIZ) nchini Tanzania Bw. Ralf Senzel na Mkuu wa Ushirikiano
wa Maendeleo kutoka Ubalozi wa Ujerumani hapa nchini Dkt. Katrin
Bornemann waliofika katika ofisi ndogo za Wizara ya Mifugo na Uvuvi
zilizopo jijini Dar es Salaam kuzungumzia mradi wa uhifadhi wa bainuai
za Bahari ya Hindi na Maeneo Tengefu ya Ukanda wa Pwani, utakaofadhiliwa
na Serikali ya Ujerumani katika kipindi cha miaka minne. (Picha na
Edward Kondela – Afisa Habari, Wizara ya Mifugo na Uvuvi)
Picha
ya pamoja ya Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi anayeshughulikia
Uvuvi Dkt. Rashid Tamatamah (wa tatu kutoka kulia), Mkuu wa Ushirikiano
wa Maendeleo kutoka Ubalozi wa Ujerumani hapa nchini Dkt. Katrin
Bornemann (kulia kwake) na Mratibu wa Shirika la Maendeleo la Ujerumani
(GIZ) nchini Tanzania Bw. Ralf Senzel (kushoto kwake), Mkurugenzi Mkuu
wa Taasisi ya Uvuvi Tanzania (TAFIRI) Dkt. Ishmael Kimirei (wa pili
kutoka kushoto), Kaimu Meneja wa Kitengo cha Hifadhi za Bahari na Maeneo
Tengefu (MPRU) (wa kwanza kushoto) na Mratibu wa Usimamizi Shirikishi
wa Rasilimali za Uvuvi Kusini Magharibi mwa Bahari ya Hindi (SWIOFish) Dkt. Nichrous Mlalila (wa kwanza kulia), mara baada ya kuhitimisha
mazungumzo ya kukazia ushirikiano baina ya Tanzania na Ujerumani hususan
katika Sekta ya Uvuvi yaliyofanyika katika ofisi ndogo za wizara
zilizopo jijini Dar es Salaam. (Picha na Edward Kondela – Afisa Habari,
Wizara ya Mifugo na Uvuvi)
Na. Edward Kondela
Katibu Mkuu Wizara
ya Mifugo na Uvuvi anayeshughulikia Uvuvi Dkt. Rashid Tamatamah
amekutana na ujumbe kutoka Ubalozi wa Ujerumani hapa nchini na Shirika
la Maendeleo la Ujerumani (GIZ) na kufanya mazungumzo ya kukazia
ushirikiano baina ya Tanzania na Ujerumani, kwenye uhifadhi wa bainuai
za Bahari ya Hindi na Maeneo Tengefu ya Ukanda wa Pwani.
Akizungumza
leo (13.05.2022) mara baada ya kukutana na ujumbe huo katika ofisi
ndogo za Wizara ya Mifugo na Uvuvi jijini Dar es Salaam, Dkt. Tamatamah
amesema katika Ukanda wa Bahari ya Hindi kutakuwa na miradi mingi ambapo
kwa kuanzia Mwezi Agosti Mwaka huu 2022, mradi utafanyika Kaskazini mwa
Tanzania katika Wilaya ya Mkinga Mkoani Tanga na Kwale Mkoani Kenya.
Katibu
mkuu huyo mara baada ya kukutana na ujumbe huo ambao ni Mkuu wa
Ushirikiano wa Maendeleo kutoka Ubalozi wa Ujerumani hapa nchini Dkt.
Katrin Bornemann na Mratibu wa Shirika la Maendeleo la Ujerumani (GIZ)
nchini Tanzania Bw. Ralf Senzel, amesema Tanzania itapata Euro Milioni
2.17 sawa na Shilingi za Kitanzania Bilioni 5.2 kwenye mradi huo katika
kipindi cha miaka minne.
“Huu mradi una faida unalenga kuhifadhi
bainuai, utatoa elimu kwa jamii inayokaa katika maeneo hayo na
tunategemea mradi utafanya rasilimali kuwa endelevu kwa muda mrefu na
utaongeza kipato kwa wananchi, kwa kuwa wataelimishwa njia mbadala za
maisha na kuhifadhi Maeneo Tengefu.” Amesema Dkt. Tamatamah.
Naye
Mkuu wa Ushirikiano wa Maendeleo kutoka Ubalozi wa Ujerumani hapa
nchini Dkt. Katrin Bornemann amesema ana furaha kwamba ushirikiano baina
ya Ujerumani na Tanzania katika maeneo ya bainuani na Maeneo Tengefu
utakuwa na nguvu katika kuhakikisha Ukanda wa Pwani wa Bahari ya Hindi
unatunzwa pamoja na kuhakikisha rasilimali zilizopo katika Maeneo
Tengefu zinaendelezwa, huku Mratibu wa Shirika la Maendeleo la Ujerumani
(GIZ) nchini Tanzania Bw. Ralf Senzel, amesema mradi huo utajenga
uhusiano mzuri baina ya nchi hizo mbili.
Mazungumzo hayo baina
ya Katibu Wizara ya Mifugo na Uvuvi anayeshughulikia Uvuvi Dkt. Rashid
Tamatamah na Mkuu wa Ushirikiano wa Maendeleo kutoka Ubalozi wa
Ujerumani hapa nchini Dkt. Katrin Bornemann pamoja na Mratibu wa Shirika
la Maendeleo la Ujerumani (GIZ) nchini Tanzania Bw. Ralf Senzel,
yamehudhuriwa pia na Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Uvuvi Tanzania
(TAFIRI) Dkt. Ishmael Kimirei, Kaimu Meneja wa Kitengo cha Hifadhi za
Bahari na Maeneo Tengefu (MPRU) Bw. John Komakoma ambapo mradi huo
utatekelezwa na Mratibu wa Usimamizi Shirikishi wa Rasilimali za Uvuvi
Kusini Magharibi mwa Bahari ya Hindi (SWIOFish) Dkt .Nichrous Mlalila.
Mwisho.