FAO NA USAID TANZANIA WAIPIGA TAFU SERIKALI KUKINGA KICHAA CHA MBWA

May 01, 2018



Naibu Waziri Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega (wa tatu kushoto) akizungumza jambo na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Chakula na Kilimo Duniani (FAO) Fred Kafeero (katikati) na Mwakilishi Shirika la Misaada la Marekani (USAID), Dk. Patrick Swai wkati wa hafla ya kukabidhiwa msaada wa chanjo ya Kichaa cha mbwa kwa kwa ajili ya kuzuia ugonjwa huo kwa Wilaya ya Moshi iliyopo mkoani Kilimanjaro, ambayo imeripotiwa kuwa na tatizo hilo hivi karibuni. Hafla hiyo imefanyika wizarani hapoleo Aprili 30 2018 jijini Dar es Salaam. (Imeandaliwa na Robert Okanda Blogs)


Kiongozi wa Timu wa FAO, Florunso Fesina akitoa mada kuhusu utafiti uliofanywa na shirika hilo kwa madhara yasababiswayo na mifugo kutopewa chanjo hasa mbwa na paka wakati wa hafla ya shirika hilo kukabidhi msaada wa chanjo ya ugonjwa wa kichaa cha mbwa kwa wizara ya Mifugo na uvuvi jjini Dar es Salaam leo.




Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Chakula na kilimo Duniani (FAO) Fred Kafeero (wa tatu kulia) na Mwakilishi shirika la Misaada la Marekani (USAID), Dk. Patrick Swai (wa pili kulia) wakionesha moja ya bango litakalotumika wakati wa tiba na na chanjo katika hafla ya kukabidhi msaada wa chanjo ya Kichaa cha mbwa kwa Naibu Waziri Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega (wa tatu kushoto) kwa ajili ya kuzuia ugonjwa huo kwa Wilaya ya Moshi iliyopo mkoani Kilimanjaro, ambayo imeripotiwa kuwa na tatizo hilo hivi karibuni. Hafla hiyo imefanyika wizarani hapo jana jijini Dar es Salaam. Pamoja nao ni watendaji waandamizi wa wizara


Sehemu ya washiriki wa hafla hiyo wakifuatilia mada.

Kiongozi wa Timu wa FAO, Florunso Fesina akitoa mada kuhusu utafiti uliofanywa na shirika hilo kwa madhara yasababiswayo na mifugo kutopewa chanjo hasa mbwa na paka wakati wa hafla ya shirika hilo kukabidhi msaada wa chanjo ya ugonjwa wa kichaa cha mbwa kwa wizara ya Mifugo na Uvuvi jjini Dar es Salaam leo.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »