Na Veronica Simba – Dodoma
Serikali
ya Tanzania kupitia Wizara ya Nishati na Kampuni ya Total wamekubaliana
kuharakisha hatua zote za awali katika Mradi wa Bomba la Mafuta kutoka
Uganda hadi Hoima Tanga ili shughuli za ujenzi rasmi zianze mwezi Mei
mwaka huu.
Makubaliano
hayo yalifikiwa Alhamisi, Februari 1, wakati Waziri wa Nishati, Dkt.
Medard Kalemani alipokutana na uongozi wa juu wa kampuni hiyo wizarani
Dodoma.
Aidha,
makubaliano mengine yaliyofikiwa katika kikao hicho ni kuwa kazi za
awali za maandalizi ya ujenzi ziwe zimekamilika ifikapo mwezi Machi
mwaka huu.
“Ni
lazima tuharakishe mchakato huu kama Mheshimiwa Rais Magufuli
alivyoagiza. Hivyo, tumekubaliana kwamba shughuli zote za maandalizi
ziwe zimekamilika ifikapo Machi mwaka huu ili kuwezesha shughuli rasmi
za ujenzi wa Bomba kuanza mwezi Mei,” alifafanua Waziri Kalemani.
Vilevile,
katika kikao hicho, Rais wa Kampuni ya Total sehemu ya Afrika, Guy
Maurice ambaye alikuwa kiongozi wa Ujumbe huo, alibainisha nia ya
kampuni yake kuwekeza katika shughuli nyingine mbalimbali zinazohusiana
na Mradi wa Bomba jambo ambalo alisema litainufaisha zaidi Tanzania.
Mbali
na makubaliano yote yaliyofikiwa, Waziri Kalemani pia alisisitiza kuwa
ni muhimu kampuni ya Total iwasilishe Mpango-Kazi wake wizarani mapema
iwezekanavyo ili utumike kama mwongozo-rejea katika kutathmini
utekelezaji wa Mradi huo mkubwa.
Kampuni ya Total ndiyo mwekezaji katika utekelezaji wa Mradi wa ujenzi wa Bomba la Mafuta kutoka Uganda hadi Hoima, Tanga.
Kikao
hicho pia kilihudhuriwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Dkt.
Hamisi Mwinyimvua, Mkurugenzi wa Utawala na Utumishi wa Wizara Lusius
Mwenda, Mkurugenzi wa Sera na Mipango Haji Janabi na maafisa wengine
waandamizi kutoka wizarani.
Waziri
wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani (katikati), akiongoza kikao baina ya
viongozi na wataalam wa Wizara (kulia) na Ujumbe kutoka Kampuni ya Total
(kushoto). Kikao hicho kilifanyika Makao Makuu ya Wizara mjini Dodoma,
Februari Mosi, mwaka huu.
Waziri
wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani, akisalimiana na Ujumbe kutoka Kampuni
ya Total kabla ya kuanza kwa kikao baina yao kujadili utekelezaji wa
Mradi wa Bomba la Mafuta kutoka Uganda hadi Hoima-Tanga. Kikao hicho
kilifanyika Makao Makuu ya Wizara mjini Dodoma, Februari Mosi, mwaka
huu.
Waziri
wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani (kushoto), akimsikiliza Rais wa
Kampuni ya Total sehemu ya Afrika, Guy Maurice (kulia) wakati wa kikao
baina yao kujadili utekelezaji wa Mradi wa Bomba la Mafuta kutoka Uganda
hadi Hoima-Tanga. Kikao hicho kilifanyika Makao Makuu ya Wizara mjini
Dodoma, Februari Mosi, mwaka huu.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Nishati, Dkt. Hamisi Mwinyimvua, akisalimiana na
Ujumbe kutoka Kampuni ya Total kabla ya kuanza kwa kikao baina ya Wizara
na Ujumbe kutoka Kampuni hiyo kujadili utekelezaji wa Mradi wa Bomba la
Mafuta kutoka Uganda hadi Hoima-Tanga. Kikao hicho kilifanyika Makao
Makuu ya Wizara mjini Dodoma, Februari Mosi, mwaka huu na kiliongozwa na
Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani.
Viongozi
na wataalam wa Wizara ya Nishati, wakiwa katika kikao baina ya Wizara
na Ujumbe kutoka Kampuni ya Total kujadili utekelezaji wa Mradi wa Bomba
la Mafuta kutoka Uganda hadi Hoima-Tanga. Kikao hicho kilifanyika Makao
Makuu ya Wizara mjini Dodoma, Februari Mosi, mwaka huu na kiliongozwa
na Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani (hayupo pichani).
Ujumbe
kutoka Kampuni ya Total wakiwa katika kikao baina yao na Viongozi na
wataalam wa Wizara ya Nishati kujadili utekelezaji wa Mradi wa Bomba la
Mafuta kutoka Uganda hadi Hoima-Tanga. Kikao hicho kilifanyika Makao
Makuu ya Wizara mjini Dodoma, Februari Mosi, mwaka huu na kiliongozwa na
Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani (hayupo pichani).