NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII JAPHET HASUNGA AWAONYA WANANCHI WA KISARAWE KUVAMIA HIFADHI

December 26, 2017

1
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga (wa tatu kulia) akiwa na baadhi ya Wakurugenzi wa Wakala wa Huduma za Misitu  Tanzania (TFS),  kutoka makao makuu  Dar es Salaam  akiangalia vitalu vya miche ya miti  wakati   alipowatembelea wanakijiji wa Maguruwe wanaopakana na msitu wa Hifadhi wa  Kazimzumbwi waliojitolea kuotesha miche ya miti  kwa ajili ya kupanda   kwenye  eneo la msitu huo uliokuwa umevamiwa takriban theluthi tatu kwa kipindi cha kuanzia mwaka 1993 hadi 2014.
2
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga (wa kwanza kulia) akipata maelezo kutoka kwa Kaimu Meneja wa Misitu wa Wilaya ya Kisarawe, Mathew Mwanuo   ( wa kwanza  kushoto)  wakati  alipofanya ziara mwishoni mwa wiki ya kutembelea  kilichokuwa  Kiwanda  cha Caoline, kilichopo katika  msitu wa hifadhi Pugu wilayani Kisarawe mkoani Pwani .
3
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga (katikati) akiwa na baadhi ya Wakurugenzi wa Wakala wa Huduma za Misitu  Tanzania (TFS),  kutoka makao makuu jijini Dar es Salaam  wakioneshwa  ramani ya Msitu wa Hifadhi Kazimzumbwi na Kaimu Meneja wa Misitu wa Wilaya ya Kisarawe, Mathew Mwanuo (  wa tatu kushoto) kuhusiana na“eneo la msitu huo lilivyokuwa limevamiwa takriban theluthi tatu kwa kipindi cha kuanzia mwaka 1993 hadi 2014.
4
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa wilaya ya Kisarawe, Viongozi wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) wakiwemo  watumishi   wakati Naibu Waziri huyo alipofanya ziara mwishoni mwa wiki  ya kutembelea  msitu wa Hifadhi wa Kazimzumbwi na Pugu wilayani Kisarawe mkoani Pwani.
5
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga (katikati)  akizungumza na wanakijiji wa Maguruwe  wanaopakana na msitu wa Hifadhi wa  Kazimzumbwi waliojitolea kuotesha miche ya miti kwa ajili ya kupanda   kwenye  eneo la msitu huo uliokuwa umevamiwa takriban theluthi tatu kwa kipindi cha kuanzia mwaka 1993 hadi 2014 wakati Naibu Waziri huyo alipofanya  ziara mwishoni mwa wiki katika msitu huo.
6
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga akisaini kitabu cha wageni alipotembelea  eneo kilichokuwa Kiwanda  cha Caoline, kilichopo  katika  msitu wa hifadhi Pugu wilayani Kisarawe mkoani Pwani wakati Naibu Waziri huyo alipofanya ziara mwishoni mwa wiki  katika msitu wa Hifadhi wa Kazimzumbwi na Pugu.
8
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga (katikati) akipatiwa maelezo na Mkurugenzi wa Rasilimali za Misitu na Nyuki wa   Wakala wa Huduma za Misitu  Tanzania (TFS), Zawadi Mbwambo  ( wa kwanza  kushoto)  wakati  alipofanya ziara jana ya   kutembelea  kilichokuwa  Kiwanda  cha Caoline, kilichopo katika  msitu wa hifadhi Pugu wilayani Kisarawe mkoani Pwani
9
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga (wa kwanza kushoto) akioneshwa eneo la msitu Kazimzumbwi na Kaimu Meneja wa Misitu wa Wilaya ya Kisarawe, Mathew Mwanuo   lilivyokuwa limevamiwa takriban theluthi tatu kwa kipindi cha kuanzia mwaka 1993 hadi 2014 wakati Naibu Waziri huyo alipofanya  ziara mwishoni mwa wiki katika msitu huo
Picha na Lusungu Helela-MNRT
……………………
NAIBU Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga amewataka wananchi wanaozunguka hifadhi za misitu katika wilaya ya Kisarawe kuzingatia mipaka iliyowekwa pamoja na matumizi ya ardhi ili kuepuka migogoro inayoweza kujitokeza baina ya wananchi na serikali.
Hasunga alisema jana kwenye ziara aliyoifanya alipotembelea Kiwanda cha Caoline, pamoja na msitu wa hifadhi Kazimzumbwi na Pugu.
Alisema serikali haitakubali kuona maeneo ya hifadhi yanavamiwa ovyo na wananchi ama mifugo kuachiliwa bila utaratibu maalum.
“Kuna umuhimu mkubwa wa kukuza sekta ya utalii. Wataalii wengi wanapenda kuona misitu. Hii ni sehemu ya utalii,” alisema.
Aliwataka Kisarawe kuangalia vivutio walivyonavyo ili kuboresha katika maeneo hayo kwa ajili ya kuvutia utalii.
Kwa upande wake Kaimu Meneja Misitu Kisarawe, Mathew Mwanuo alisema wilaya hiyo ina misitu minne ya hifadhi ya serikali Kuu ambayo ni Ruvu Kusini, Masanganya, Pugu na Kazimzumbwi.
Alisema msitu wa Kazimzumbwi umekuwa ukivamiwa mara kwa mara na watu kutoka maeneo mbalimbali hasa jijini Dar es Salaam.
“Msitu huu ulikuwa umevamiwa takriban theluthi tatu kwa kipindi cha kuanzia mwaka 1993 hadi 2014. Hata hivyo wavamizi hao waliendelea kuvamia kwa nyakati tofauti hadi mwaka huu,” alisema.
Alisema walianza kuwaondoa mwishoni mwa Agosti mwaka huu, Kamati ya Ulinzi na Usalam ya wilaya ya Kisarawe kwa kushirikiana na maofis wa Wakala wa Huduma za misitu Tanzania walianza kutembelea eneo la msitu kuangalia uvamizi na uharibifu uliofanyika katika Msitu wa Hifadhi wa Kazimzumbwi ikiwa ni pamoja na kuona ukubwa wa uharibifu na namna ya kutekeleza zoezi.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »