Naibu
Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI) Joseph
Kakunda akipima kiasi cha saruji kilichowekwa kwenye mchanga katika ujenzi
shule ya Sekondari Iguguni Wilayani Mkalama katika ziara yake ya Siku moja
kufuatilia utoaji huduma mbalimbali kwa jamii.
Naibu
Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI) Joseph
Kakunda akisisitiza jambo mbele ya Mkuu wa Wilaya ya Mkalama Mhandisi Jakson
Masaka (kulia kwake) na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama
Mhandisi Godfrey Sanga (kushoto kwake).
Naibu
Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI) Joseph
Kakunda akisalimiana na mwenyeji wake Mkuu wa Wilaya ya Mkalama Mhandisi
Jaksoni Masaka mara baada ya kuwasili wilayani humo kwa ajili ya Ziara ya
ufuatiliaji wa miradi ya elimu na maji.
Naibu
Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI) Joseph
Kakunda akisalimiana na Katibu Tawala wa Wilaya ya Mkalama Elizabeth Rwegasira
mara baada ya kuwasili wilayani humo kwa ajili ya Ziara ya ufuatiliaji wa
miradi ya elimu na maji.
Naibu
Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI) Joseph
Kakunda ameziagiza halmashauri zote nchini kutumia mafundi wa kawaida wazawa
waliopo katika maeneo yao katika miradi yote midogo kupitia utaratibu
unaojulika kama ‘force account’.
Naibu
Waziri Kakunda ametoa agizo hilo jana mara baada ya kufanya ziara Wilayani
Mkalama kufuatilia utoaji wa huduma mbalimbali kwa jamii huku akijikita zaidi
katika sekta ya Maji na Elimu, ambapo ametembelea mradi wa maji Iguguno na Shule
ya Sekondari Iguguno.
“Matumizi
ya Wakandarasi yabaki katika miradi mikubwa tu lakini miradi yote midogo
tuwatumie mafundi waliopo katika maeneo yetu, mafundi hawa wazawa wanatekeleza
kazi kwa ubora kama huu ambao nimeuona leo na kwa gharama ambazo ni nzuri,”
amesisitiza mara baada ya kutoa agizo hilo.
Ameeleza
kuwa gharama na ubora wa mradi wa Shule ya Sekondari ya Iguguno ambao
unajumuisha ujenzi na ukarabati wa madarasa 8, mabweni mawili, vyoo vyenye
matundu 11, bwalo la chakula na maabara ambapo vyote hivyo vimegharimu milioni
416, unatosha kudhirihisha kuwa mafundi wa kawaida wazawa wanaweza kufanya kazi
nzuri.
“Huu
mradi endapo tungetumia utaratibu wa wakandarasi na wazabuni hiyo gharama ya
milioni 416 ingekuwa kama robo ya gharama, nasisitiza wakandarasi na wazabuni
watumike katika miradi mikubwa tu”, Naibu Waziri Kakunda amesisitiza.
Ameongeza
kwa kuipongeza halmashauri hiyo kwa kutekeleza mradi mkubwa wa maji ambao
umewezesha usambazaji wa maji katika kata yote ya Iguguno na kuwasaidia
wananchi wasihangaike kupata maji.
Aidha
Naibu Waziri Kakunda ameonekana kutofurahishwa na taarifa kuhusu wanafunzi 12
waliokatishwa masomo tangu mwezi Januari Mwaka huu kutokana na sababu ya kupewa
ujauzito, ambapo ametoa rai kwa wazazi na walezi wote nchini kuwa mstari wa
mbele kukomesha tatizo hilo.
Ameeleza
kuwa wazazi wengi wamekuwa wakifanya makubaliano ambapo mwanafunzi aliyepewa
ujauzito anamkana mhalifu aliyempa ujauzito ili kumuepusha na kifungo cha miaka
30 jela, jambo linalofanya kesi nyingi kukosa ushahidi huku tatizo la mimba kwa
wanafunzi likiendelea kuwepo.
Naibu
Waziri Kakunda amesema ili kukomesha hilo serikali kupitia Wizara yake ina
dhamira ya kupeleka hati ya dharula bungeni ili itungwe sheria itakayofuta
dhamana ya mtuhumiwa atakayempa ujauzito mwanafunzi huku uchunguzi wa Vinasaba
(DNA) utatakiwa kufanyika ili kuthibisha kama mtuhumiwa ndiye baba wa mtoto ama
la.
Awali,
Mbunge wa jimbo la Mkalama Mhe. Alan Kiula amewasilisha changamoto mbalimbali
za Wilaya hiyo kwa Naibu Waziri Kakunda kwa kumueleza changamoto kubwa ni
kutokuwa na hospitali ya Wilaya.
Mhe.
Kiula ameongeza kuwa upungufu wa watumishi katika Wilaya hiyo hasa wa Sekta ya
Elimu na Afya umekuwa ukikwamisha baadhi ya shughuli kufanyika kwa kasi
inayotakiwa.
Aidha
amemshukuru Naibu Waziri Kakunda kwa ahadi yake ya kuitazama Wilaya hiyo kwa
jicho la pekee katika mgao ujao wa watumishi kwa Mwezi Disemba na Januari huku
akimuhakikishia kuwa Halmashauri itafanya kwa haraka taratibu za awali za upatikanaji
wa eneo kwa ajili ya ujenzi wa hospitali ya Wilaya.
EmoticonEmoticon