“HATUWEZI KUJUTA UWEPO WA MBUNGE AMBAYE TUMEMCHAGUA –CUF TANGA”

September 26, 2017
Mbunge wa Jimbo la Tanga (CUF) Alhaj Mussa Mbaruku akizungumza na waandishi wa habari kulia ni Katibu wa CUF wilaya ya Tanga,Thobias Haule
Naibu Meya wa Jiji la Tanga (CUF) Mohamed Haniu akizungumza kushoto ni Mbunge wa Jimbo la Tanga,Alhaj Mussa Mbaruku kulia ni Katibu wa CUF wilaya ya Tanga,Thobias Haule
Diwani wa viti maalumu (CUF) akizungumza
 Sehemu ya wanachama wa chama hicho wakifuatilia mkutano huo

 CHAMA cha Wananchi CUF wilaya ya Tanga kimekanusha uvumi unaoonezwa kuwa wanajuta uwepo Mbunge wa Jimbo la Tanga (CUF) Alhaj Mussa Mbaruku huku kikiwataka wananchi kuwapuuza wanaoeneza taarifa hizo.

Hata hivyo amesema wamesikitishwa na kauli zinazoelezwa kuwa chama
  hicho kinawaomba radhi wananchi wa Jiji hilo kutokana na mbunge huyo kutokuwa na uwakilishi mzuri bungeni kwani tokea apewe nafasi hiyo amekuwa hodari na shupavu kusimamia maendeleo ya Jimbo hilo.

Hayo yalibainishwa leo na Katibu wa Chama cha CUF wilaya ya

Tanga,Thobias Haule wakati wa mkutano wao na waandishi wa habari uliofanyika jana mjini hapa uliohudhuriwa na mbunge huyo na wanachama wa chama hicho ambapo alisema kuna mambo yanayofanyika ni yasiyokuwa na tija ndani ya chama hicho.

Alisema wao wamechaguliwa kuhakikisha wanawatumikia wananchi na sio
  kutunishia misuli jambo ambalo linaweza kupelekea kushindwa kuwatumikia wananchi.

“Ndugu zangu waandishi kuna mambo yanafanyika ya kihuni na ndani ya
  CUF Uhuni hauna nafasi nisema Jiji la Tanga limetulia na Mbunge anafanya kazi na madiwani nao pia ….sisi tumechaguliwa kwa maslahi ya Tanga na sio vyenginevyo “Alisema.

“Kwanza hatujakaa kikao chohote na hatujasema tunaomba radhi wakazi wa
  Jiji la Tanga eti Mbunge Mussa hana uwezo  ...eti hafai tumeshuhudia wabunge wengi wa miaka ya nyuma ambao walikuwa hawaeleze changamoto za  wananchi kwenye vikao vya bunge lakini huyu tunaona namna anavyopambana.

Naye Mwanachama wa chama hicho,Jumbe Zahoro alisema wamesikitishwa
  sana na kauli kuwa wao wanasikitika kwa sababu hawawezi kusikitika kwa kiongozi ambaye wamemteua na baadae kumpigana mpaka atachaguliwa kuliongoza jimbo hilo.

“Nimesikishwa kuona mtu anasimama na kueleza maneno anayoyataka  kwa
  sababu chama hicho kina kanuni na katiba  haiwezekani mtu anasimama na kusema tunasikitika kwa mbunge ambaye tumemchagua bila kuangalia chama hicho ni cha watu hilo jambo sio kweli “Alisema.

Alisema sio kweli wao CUF wanasikitika kwa mtu ambaye tumeanza kumteua
  na baadae kuanza kumchagua jambo ambalo haliwezi kuwaingia akilini watu.

Awali akizungumza,Mbunge Mussa alisema hivi sasa dhamira kubwa ni
  kuhakikisha anawatumikia wananchi kwa moyo mmoja ili kuweza kusogeza mbele gurudumu la maendeleo kama ilivyokuwa miaka ya nyuma.

“Tanga imerudisha heshima yake kwa kuanza kupokea miradi mbalimbali
  mikubwa ambayo kwa namna moja au nyingine itakuwa mkombozi kwa wakazi wa Tanga hata mikoa ya jirani hii ni ishara tosha sasa tunarudi kwenye enzi zetu za viwanda “Alisema.

Alisema matarajio hayo hivi sasa yanakwenda sambamba na ujio wa miradi
  ya Bomba la mafuta,ujenzi wa kiwanda cha saruji eneo la Amboni kitakachomilikiwa na Wachina,ujenzi wa barabara ya
Tanga-Pangani-Saadan hadi Bagamoyo.

Alisema miradi hiyo itafungua fursa za kiuchumi kwa mkoa wa Tanga huku
  akiwataka wananchi kujiandaa kuchangamkia fursa hizo kwa ili kuweza kujikomboa kwa kuanzisha shughuli mbalimbali ikiwemo ujasiriamali.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »