Tigo yatoa smartphone 120 katika kampeni ya kusisimua

August 12, 2017



Ofisa Mzinduzi wa Bidhaa za Tigo, Jacqueline Nnunduma, akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, wakati wa kukabidhi zawadi kwa washindi wa promosheni ya Jaza Ujazwe Ujaziwe Zaidi iliyofanyika jijini Dar es Salaam. 

Ofisa Mzinduzi wa Bidhaa za Tigo, Jacqueline Nnunduma (kushoto), akimkabidhi simu aina ya S1 mmoja kati ya washindi 120 wa promosheni ya Jaza Ujazwe Ujaziwe Zaidi, Margteth Taumbe katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam. 

Ofisa Mzinduzi wa Bidhaa za Tigo, Jacqueline Nnunduma (kushoto), akimkabidhi simu aina ya S1 mmoja kati ya washindi 120 wa promosheni ya Jaza Ujazwe Ujaziwe Zaidi, Pili Mohamed katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam.

Ofisa Mzinduzi wa Bidhaa za Tigo, Jacqueline Nnunduma (kushoto), akimkabidhi simu aina ya S1 mmoja kati ya washindi 120 wa promosheni ya Jaza Ujazwe Ujaziwe Zaidi, Rajabu Ngorongo katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam. 

Dar es Salaam. Agosti 11, 2017- Tigo Tanzania, mtandao unaoongoza kwa maisha bora ya kidijitali, inaendelea kuwazawadia wateja wake na kwa wakati huu imezawadia  wateja wake 120 na  simu mpya  za mkononi za  smartphone Tecno S1. Hii ni sehemu ya kampeni inayoendelea ya Jaza Ujazwe Ujaziwe Zaidi   kwa wiki ya kwanza ya Agosti.

Akizungumza kwenye hafla ya kutoa zawadi  kwa washindi wa Dar es Salaam,  Afisa Mzinduzi wa Bidhaa za Tigo, Jacqueline Nnunduma,   alibainisha kuwa tofauti na promosheni nyingine   ambapo wateja wachache tu wanapata zawadi, Tigo inatoa simu moja ya Tecno S1, kila saa kwa masaa 24 kila siku ya wiki kwa muda wote wa kampeni hiyo ya kusisimua.

"Promosheni ya Tigo Jaza Ujazwe, Ujaziwe Zaidi ni bora zaidi na tofauti na promosheni nyingine kwa sababu kila mteja anapata zawadi kila mara anapoongeza muda wa maongezi . Kwa kuongeza salio tu, kila mteja pia anapata nafasi ya kushinda simu moja ya Tecno S1 smartphone inayoshindaniwa kila saa ya kila siku, kwa siku saba za wiki. Washindi wa simu ya smartphone ya Tecno S1 pia watafurahia mawasiliano ya bure ya simu kwa mwaka mmoja. Zawadi nyingine anazoweza kushinda mteja ni pamoja na  bonasi ya bure kwenye huduma ya sauti, data na ujumbe mfupi wa maneno  SMS kulingana na matumizi ya mteja husika, "alisema.
Kwa mujibu wa Tigo, jumla ya simu za mkononi  720 zipo tayari  kunyakuliwa  katika promosheni  inayoendelea sasa ya Jaza Ujazwe Ujaziwe Zaidi.   Wateja wanaweza kushinda simu za mkononi kila saa kirahisi  kwa kuongeza muda wa maongezi  wa Tigo kupitia kadi za kukwangua, e-pin au TigoPesa, ambapo namba yao ya simu itaingia kwenye droo  ya  nafasi ya kushinda moja ya simu za mkononi zinazoshindaniwa kila saa , ya kila siku kwa siku saba za wiki.
  Aliendelea kuongeza  kuwa Waratibu  wa Biashara na Masoko wa Tigo tayari wamejiandaa kukabidhi simu  za smartphones kwa washindi wengine wa droo ya wiki hii waliopatikana kutoka   Dodoma, Tanga, Kagera, Kilimanjaro, Lindi, Mbeya, Morogoro, Mtwara, Mwanza, Singida, Tanga na Zanzibar.
"Kama kawaida, Tigo inasikiliza na kuitikia   mahitaji ya wateja wake, na sasa tunawapatia zawadi kemkem kama njia mojawapo ya kuwashukuru kwa kuendelea kutumia bidhaa na huduma zetu bora. Nachukua fursa hii kuwakumbusha wateja wote wa Tigo kwamba zawadi ni nyingi na wote wanaoshiriki wanashinda zawadi, kwa hiyo  wachangamkie fursa hii ya kusisimua ya kuvuna zawadi kupitia promosheni ya Jaza Ujazwe Ujaziwe Zaidi ", alisema Nnunduma.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »