.Moja ya kikundi cha Timu ya Mauzo Tigo wakiwa katika picha ya pamoja katika maonesho ya Kilimo yanayoendelea Mkoani Lindi. |
· Wakati maadhimisho haya yanafanyika mkoani Lindi kitaifa, Tigo inashiriki kikamilifu katika maadhimisho ya Nanenane katika mikoa ya Morogoro, Mbeya, Dodoma, Arusha, Mwanza na Tabora.
· Pia kama ilivyo kawaida yetu ya kuwajali wateja na wananchi kwa ujumla kupitia bidhaa na Huduma zetu bora, kupitia msimu huu wa Nanenane tunatoa ofa kabambe kuhakikisha wananchi wanaendelea kufurahia maisha ya kidigitali. Ofa hizi ni kwa simu za kijanja aina ya Tecno S1 kwa bei ya TZS 99,000/- na Tecno R6 kwa bei ya TZS 195,000 tu. Unaponunua simu hizi unapata mpaka GB 3 za kuperuzi na mtandao ulioboreshwa zaidi Tanzania.
· Hii ni sababu tosha kwa wakazi wote wa Lindi na mikoa mingine ambapo maonyesho haya ya Nanenane yanaendelea kuwahi katika banda la Tigo na kujinyakulia simu ili kupata nafasi ya kujishindis Zawadi tulizozitaja.
Hayo yalisemwa na Meneja Mauzo wa Tigo mkoa wa Mtwara, Lilian Mwalongo kwenye maonesho hayo jana
EmoticonEmoticon