Mwanasheria
wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Oscar Mangula akiwasilisha mada inayohusu
Sheria mpya ya Takwimu ya mwaka 2015 wakati wa mafunzo kwa Maafisa
Habari na Mawasiliano Serikalini yaliyofanyika leo mkoani Morogoro kwa
ajili ya kuwajengea uwezo wa kuifahamu Sheria mpya ya Takwimu ya mwaka
2015.
Meneja
wa Idara ya Mbinu za kitakwimu, Viwango na Uratibu kutoka Ofisi ya
Taifa ya Takwimu, Emilian Karugendo akitoa ufafanuzi wa namna Ofisi ya
Taifa ya Takwimu inavyokusanya takwimu rasmi nchini kwa kuzingatia
kanuni za kitaifa na kimataifa wakati wa mafunzo kwa Maafisa Habari na
Mawasiliano Serikalini yaliyofanyika leo mkoani Morogoro kwa ajili ya
kuwajengea uwezo wa kuifahamu Sheria mpya ya Takwimu ya mwaka 2015.
Baadhi
ya Maafisa Habari na Mawasiliano Serikalini wakifuatilia uwasilishwaji
wa mada wakati wa mafunzo kwa Maafisa hao yaliyofanyika leo mkoani
Morogoro kwa ajili ya kuwajengea uwezo wa kuifahamu Sheria mpya ya
Takwimu ya mwaka 2015.
Baadhi
ya Maafisa Habari na Mawasiliano Serikalini wakifuatilia uwasilishwaji
wa mada wakati wa mafunzo kwa Maafisa hao yaliyofanyika leo mkoani
Morogoro kwa ajili ya kuwajengea uwezo wa kuifahamu Sheria mpya ya
Takwimu ya mwaka 2015.
………………………………
Na: Emmanuel Ghula
Morogoro
1 Juni, 2017.
OFISI
ya Taifa ya Takwimu (NBS) imetoa mafunzo kwa Maafisa Habari na
Mawasiliano Serikalini leo mkoani Morogoro kuhusu Sheria ya Takwimu ya
mwaka 2015 ili kuwajengea uwezo wa kufahamu namna sheria hiyo
inavyofanya kazi.
Akifafanua
sheria hiyo, Mwanasheria wa NBS, Oscar Mangula amesema sheria ya
Takwimu No. 9 ya mwaka 2015 imeipa Ofisi ya Taifa ya Takwimu jukumu la
kuratibu na kusimamia ukusanyaji wa takwimu rasmi nchini.
“Sheria
ya Takwimu No. 9 ya mwaka 2015 ni sheria inayoipa NBS jukumu la
kuratibu na kusimamia shughuli zote za upatikanaji wa takwimu rasmi
nchini. Hivyo, kama taasisi yoyote inataka kufanya utafiti kwa minajili
ya kutoa takwimu rasmi ni lazima iwasiliane na NBS ili kupata miongozo
ya ukusanyaji wa takwimu rasmi,” amesema Mangula.
Mangula
amesema kuwa, ni kosa kisheria kwa mtu yeyote ama taasisi kuendesha
utafiti na kuchapisha au kutoa takwimu rasmi bila kuwasiliana na NBS
kwani inaweza kukusanya takwimu ambazo hazina ubora na zinazoweza
kupotosha umma.
Aidha,
Meneja wa Takwimu za Kodi kutoka NBS Fred Matola amesema NBS hutoa
takwimu rasmi kwa kuzingatia miongozo ya kitaifa na kimataifa
inayotolewa na Umoja wa Mataifa ili kukidhi mahitaji ya nchi pamoja na
kutumika kimataifa.
“Takwimu
rasmi zinakusanywa kwa kuzingatia miongozo inayotolewa na umoja wa
kimataifa ili kukidhi mahitaji ya nchi, hivyo NBS ina wajibu kisheria
kusimamia upatikanaji wa takwimu rasmi nchini”, amesisitiza Matola.
Ofisi ya Taifa ya Takwimu ina jukumu la kuratibu na kusimamia ukusanyaji, uchambuzi na upatikanaji wa takwimu rasmi nchini.
EmoticonEmoticon