Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein
(kushoto) alipokuwa akitoa maelezo kwa Mkurugenzi wa Idara ya Ujenzi
wa Barabara katika Wizara ya Ujenzi,Mawasiliano na Usafirishaji Nd,Ali
Twahir leo wakati alipotembelea Bonde la Kibonde Mzungu kutoka na
Mafuriko yalitokea hivi karibuni kutoka na mvua kubwa za Masika
zinazoendelea kunyesha,[Picha na Ikulu.]14/05/2017.
Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein
(wa tatu kushoto) alipokuwa akiangalia maji ya Mvua yaliyofurika katika
bonde la Mwanakwerekwe nyumba mbili leo kutokana na ujenzi holela wa
Nyumba za Wananchi zilizojengwa na kupelekea kutopitisha maji katika
njia inayoelekea Ziwa Maboga, kutokana na mvua kubwa za Masika
zinazoendelea kunyesha.
Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein
(wa pili kulia) alipokuwa akiangalia maji yanayopita katika barabara ya
Mwera gudini – Fuoni meli saba leo wakati alipokuwa katika ziara ya
kutembelea maoneo mbali mbali yaliyopatwa na maafa ya Mvua za masika
zinazoendelea kunyesha (katikati) Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi
Mhe,Ayoub Mohamed Mahmoud.
Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (
kushotio) alipokuwa akizungumza na Wananchi wa Kijiji cha Bumbwisudi
leo wakati alipofika kuwariji na kuwapa pole kutokana na Nyumba zo
kuingiliwa na maji ya mvua wakati alipokuwa katika ziara ya kutembelea
maoneo mbali mbali yaliyopatwa na maafa ya Mvua za masika zinazoendelea
kunyesha (wa pili kushoto) Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Mhe,Ayoub
Mohamed Mahmoud.
Pichani
ni maji ya Mvua yakiwa yamefurika na kupelekea kufunga njia ambapo
wananchi na magari hupita kwa taabu kubwa katika barabara ya Bonde la
Kibonde Mzungu,wakati leo Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein ( hayupo pichani) alitembelea eneo hilo
akiwa na ujumbe wake katika ziara maalum,[Picha na Ikulu.]14/05/2017.
Pichani
ni Nyumba zinazojengwa eneo la Nyumba mbili Mwanakwerekwe ambapo hali
hii hupelekea kuzipa kwa mtaro wa maji ya Mvua yanayoelekea ziwamaboga
na kusababisha kuziba kwa barabara ya Mwanakwerekwe-Fuoni hatua mabyo
kusababisha usumbufu kwa wananchi wanaotumia barabara hiyo,ambapo Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (
hayupo pichani) leo alitembelea eneo hilo akiwa na ujumbe wake katika
ziara maalum.
Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (
wa pili kulia) alipokuwa akipata maelezo kutoka kwa Mkuu ya Idara ya
Mipango Miji,Kazi na Ujenzi katika Baraza la Manispaa ya Zanzibar
Nd,Mzee Khamis Juma wakati alipotembelea Mtaro wa kaji machafu katika
shehia ya Chumbuni alipokuwa katika ziara ya kutembelea maoneo mbali
mbali yaliyopatwa na maafa ya Mvua za masika zinazoendelea kunyesha.
Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein
(katikati) alipokuwa akitoa maelekezo kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya
Ujenzi,Mawasiliano na Usafirishaji Nd,Mustafa Aboud Jumbe (kulia)
alipotembelea barabara ya Mwera gudini – Fuoni meli saba leo wakati
alipokuwa katika ziara ya kutembelea maoneo mbali mbali yaliyopatwa na
maafa ya Mvua za masika zinazoendelea kunyesha (kushoto) Mkuu wa Mkoa wa
Mjini Magharibi Mhe,Ayoub Mohamed Mahmoud.
Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein
(katikati)alipokuwa akiangalia ramani inayoonesha utaratibu wa Ujenzi wa
Mitaro kutoka kwa Mkuu ya Idara ya Mipango Miji,Kazi na Ujenzi katika
Baraza la Manispaa ya Zanzibar Nd,Mzee Khamis Juma (kulia) wakati
alipotembelea Bonde la Maji mwanakwerekwe leo akiwa katika ziara maalum
ya kutembelea maoneo mbali mbali yaliyopatwa na maafa ya Mvua za
masika zinazoendelea kunyesha (kushoto) Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe,Mohamed Aboud Mohammed,[Picha na
Ikulu.]14/05/2017.
EmoticonEmoticon