Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa amewataka
wadau wa usafirishaji kuweka mikakati dhabiti ya kupunguza ajali za barabarani nchini
ili kuokoa maisha ya watanzania wanaofariki dunia kila mwaka kutokana na ajali hizo.
Waziri Mbarawa ametoa agizo hilo alipofungua mkutano maalumu wa kanda wa kujadili
na kutathmini changamoto za usalama barabarani na jinsi ya kuzikabili unaofanyika jijini
Dar es salaam.
Profesa Mbarawa amesema kuwa ajali za barabarani zimekuwa zikikatisha maisha ya
watanzania wengi kila mwaka ambao wengi wao ni vijana na nguvu kazi ya taifa hivyo
ni jukumu la wadau kubadilisha hali ya usalama barabarani.
“Kama tukijifunza vizuri na kuyafanyia kazi mafunzo haya tunaweza kubadili hali ya
usalama barabarani kwani inaumiza kuona vifo vya watu wengi vinavyotokana na ajali
za barabarani hivyo ni wakati wa Jeshi la Polisi, na Mamlaka ya Usafiri wa nchi Kavu
na Majini SUMATRA kushirikiana kukomesha ajali hizi”. Amesisitiza Profesa Mbarawa.
Ameongeza kuwa Serikali itatoa kipaumbele kwa yale yatakayojadiliwa na kuamuliwa
katika mkutano huo ili kuongeza kasi ya udhibiti wa ajali za barabarani hapa nchini na
kupunguza idadi ya ajali zinazoepukika.
Naye Mwenyekiti wa Mfuko wa Barabara nchini (RFB), Bw. Joseph Haule amesema
kuwa Bodi hiyo inashirikiana na taasisi nyingine katika kuhakikisha ubora wa
miundombinu ya barabara inakuwa salama na kupitika wakati wote.
Kwa upande wake Kamanda wa kikosi cha usalama barabarani hapa nchini Mohamed
Mpinga amesema kikosi cha usalama barabarani kitaendelea kuhakikisha kuwa ajali za
barabara zinadhibitiwa.
“Suala la ajali za barabarani ni jukumu letu sote kwa pamoja hivyo tukiungana kwa
pamoja na kushirikiana tutaweza kupunguza ajali hizi kwa kiwango kikubwa”.
Amesema Kamanda Mpinga.
Mkutano huo wa siku mbili ulioanza leo jijini Dar es salaam umewakutanisha wadaau
mbalimbali wa kimataifa wa masuala ya ujenzi na usimamizi wa usalama wa watu na
mali wawapo barabarani .
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akizungumza
na wadau waliohudhuria mkutano wa siku mbili wa Usalama barabarani
katika ukumbi wa Mwl. Julius Nyerere jijini Dar es salaam.
Mwenyekiti
wa Bodi ya Mfuko wa Barabara nchini (RFB) Bw. Joseph Haule akitoa
taarifa ya udhibiti wa ajali za barabarani kwenye mkutano wa wadau wa
usalama barabarani uliofanyika jijini Dar es salaam.
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (Kulia)
akiongea na Naibu Waziri wa Ujenzi na Mawasiliano wa Namibia Mhe.
Sankwasa James Sankwasa wakati wa mkutano wa siku mbili wa kutathmini
usalama barabarani, Jijini Dar es Salaam.
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (Kulia)
akizungumza na Mwenyekiti wa Chama cha Kimataifa kinachoshughulika na
masuala ya barabara Dkt. Kiran Kapila wakati wa mkutano wa siku mbili
wa kutathmini usalama barabarani, Jijini Dar es salaam.
Mmoja
wa wanafunzi aliyeshinda tuzo ya uchoraji wa picha ya usalama barabarani
Veronica Shirima akitoa maelezo kwa wadau wa usalama barabarani, Jijini
Dar es Salaam.
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (Wanne kulia)
akiwa katika picha ya pamoja na wadau wa Usalama barabarani mara baada
ya kufungua mkutano huo, Jijini Dar es salaam.
EmoticonEmoticon