“MPINA: AMTAKA MKANDARASI WA UJENZI WA UKUTA WA MTO PANGANI KUUKAMILISHA KWA WAKATI”

March 06, 2017

NAIBU Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira,Luhaga Mpina akisisitiza jambo wakati akizungumza na Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Martine Shigella mara baada ya kutua mkoani Tanga kwa ajili ya ziara ya kutembelea ukuta wa mto Pangani kuona namna ulivyo ambao ujenzi wake unatarajiwa kukamilika kwa kipindi cha miezi 10

NAIBU Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira,Luhaga Mpina wa pili kulia akiteta jambo na Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Martine Shigella kushoto mara baada ya kuwasili mkoani hapa kwa ajili ya ziara ya siku moja kutembelea ujenzi wa Mto Pangani kulia ni Katibu Tawala Msaidizi wa Mkoa wa Tanga,Monica Kinala

NAIBU Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira,Luhaga Mpina kulia akilakiwa na Mbunge wa Jimbo la Pangani (CCM) Jumaa Aweso mara baada ya kuwasili wilayani Pangani kwa ajili ya ziara ya siku moja kukagua ujenzi wa mto Pangani kulia ni Mkuu wa wilaya ya Pangani Zainabu Issa.

NAIBU Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira,Luhaga Mpina akiwa na mwenyeji wake Mbunge wa Jimbo la Pangani (CCM) Jumaa Aweso wakiingia kwenye ofisi ya Mkuu wa wilaya Pangani Zainabu Issa anayewaongoza mbele wakati alipowasili kwa ajili ya ziara ya kikazi ya siku moja

NAIBU Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira,Luhaga Mpina wa pili kushoto aliyevaa shati la njano akimsikiliza kwa umakini Mbunge wa Jimbo la Pangani (CCM) Jumaa Aweso wakati alipofanya ziara ya siku moja kutembelea wilaya hiyo kuangalia ukuta wa mto Pangani

 Mkuu wa wilaya ya Pangani,Zainabu Issa akitoa taarifa za Mradi wa Ujenzi wa Ukuta wa Mto Pangani kwa
NAIBU Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira,Luhaga Mpina kulia ambaye alifanya ziara ya kutembelea ukuta wa Mto Pangani ambao ujenzi wake unatarajiwa kuanza wakati wowote

NAIBU Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira,Luhaga Mpina akizungumza na watumishi wa Halamshauri ya wilaya ya Pangani leo mara baada ya kufanya ziara ya siku moja kukagua ukuta wa Mto Pangani kushoto ni Mbunge wa Jimbo la Pangani (CCM) Jumaa Aweso na kulia ni Mkuu wa wilaya ya Pangani Zainabu Issa
 Afisa Misitu wa wilaya ya Pangani,Twahiru Mkongo akielezea jambo kwa
NAIBU Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira,Luhaga Mpina wakati wa ziara yake wilayani humo
 Afisa Mazingira kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais Cletus Shengena akieleza jambo kwa
NAIBU Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira,Luhaga Mpina


NAIBU Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira,Luhaga Mpina wa tatu kutoka kushoto akiteta jambo na Mbunge wa Jimbo la Pangani (CCM) Jumaa Aweso wakati wa ziara yake wilayani humo
 Mhandisi wa Mradi kutoka Kampuni ya Dezo Civil Contractor,Daudi Abdallah  akimueleza jambo
NAIBU Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira,Luhaga Mpina kushoto ni Mbunge wa Jimbo la Pangani (CCM) Jumaa Aweso

NAIBU Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira,Luhaga Mpina akisisitiza jambo kwa
Mhandisi wa Mradi kutoka Kampuni ya Dezo Civil Contractor,Daudi Abdallah  kushoto ni Mbunge wa Jimbo la Pangani (CCM) Jumaa Aweso
 Afisa Mazingira kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais Cletus Shengena akisisitiza jambo kwa
NAIBU Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira,Luhaga Mpina kushoto namna mradi huo unavyotekelezwa

NAIBU Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira,Luhaga Mpina kulia akimsikiliza kwa umakini Afisa Mazingira ofisi ya Makamu wa Rais,Cletus Shengena alipokuwa akimueleza jambo

NAIBU Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira,Luhaga Mpina akitoka kukagua eneo ambalo kutaanza ujenzi wa ukuta wa mto Pangani wakati wa ziara yake

NAIBU Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira,Luhaga Mpina kushoto akimsikiliza kwa umakini
Mhandisi wa Mradi kutoka Kampuni ya Dezo Civil Contractor,Daudi Abdallah wakati wa ziara yake wilayani Pangani leo
NAIBU Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira,Luhaga Mpina kushoto akimsikiliza kwa umakini Mbunge wa Jimbo la Pangani (CCM) wakati alipofanya ziara ya kutembelea ukuta wa Mto Pangani.

NAIBU Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira,Luhaga Mpina amemuagiza Mkandarasi anayetekeleza mradi wa ujenzi wa ukuta wa Mto Pangani kuhakikisha mradi huo unakamilika kwa kipindi cha miezi kumi ili kuweza kuuepusha mji huo kutoweka kutokana na mabadiliko ya tabia ya nchi.
Mpina aliyema hayo jana wakati alipofanya ziara ya kutembelea ukuta wa mto Pangani ambao unatarajiwa kuanza ujenzi wake kutokana na uliokuwepo zamani kuliwa na maji kutokana na mabadiliko hayo.
Alisema kuwa mradi huo ambao utagharimu kiasi cha sh.bilioni 2.4 wenye urefu wa mita 950 ambapo ujenzi huo tayari umekwisha kuanza tokea February mwaka huu na unatarajiwa kukamilika Novemba mwaka huu.
Naibu Waziri huyo aliwataka wakandarasi hao kutekeleza ujenzi huo kwa umakini mkubwa ili thamani halisi ya fedha zinazotumika ziweze kuonekana na kuweza kuwasaidia wananchi wa mji huo wa Pangani.
“Huu mradi ni mkubwa na tumezoea kuona asilimia kubwa ya miradi kama hii inatekelezwa chini ya kiwango lakini niwaambie kuwa hatumvulimia mtu yoyote atakayoonekana kukwanisha juhudi hizi”Alisema.
Awali akizungumza katika ziara hiyo, Mbunge wa Jimbo la Pangani (CCM) Jumaa Aweso alimuomba Naibu Waziri Mpina kulitupia macho pia eneo la Pangadeco ambalo limeathiri kwa kiasi kikubwa na hatarishi kwa maisha ya wananchi.
Alisema hatari hiyo inatokana kina cha bahari kuongezeka na kusababisha eneo la makazi ya wananchi kupungua siku hadi siku na kupelekea hofu kwa jamii ya watanzania wanaoishi pembezoni mwa bahari hiyo.
“Mh Naibu Waziri awali kulikuwa na tathimini ya eneo la Pangani Kaskazini lenye urefu wa mita 950 lakini wakati suala hilo linafanyika miaka ya nyuma ikiwa eneo la Pangadeco limesahaulika na ndipo kwenye athari kubwa zaidi hivyo tunakuomba Mh uliangalie hili”Alisema.
 Sambamba na hayo lakini pia Mbunge huyo alimuomba Naibu Waziri huyo wakati utekelezaji wa mradi huo vijana wa wilaya ya Pangani waweze kunufaika na ajira ambayo ndio sera ya serikali.
“Mh Naibu Waziri tunakuomba mradi huu uwe na manufaa kwa wananchi wa wilaya ya Pangani hasa vijana waweze kupata ajira kwenye mradi huo na kuwakwamua na ugumu wa maisha “Alisema.
Naye, Mhandisi wa Kampuni ya Dezo Civil Contractor inayotekeleza mradi huo, Mhandisi Joseph mhina alisema tayari wamekwisha kupata kibali kutoka Halmashauri ya wilaya ya Pangani hivyo wanatajia kukamilisha mradi huo kama ilivyopangwa “Alisema.
Kwa upande wake, Mkuu wa wilaya ya Pangani, Zainabu Issa aliiomba serikali iwekeze nguvu kwenye mji huo ambao upo chini ya usawa wa bahari na hivyo kuathiriwa na mabadiliko ya tabia ya nchi kila wakati.


Share this

Related Posts

Previous
Next Post »