Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF),
Jamal Emil Malinzi, ametuma rambirambi kwa familia ya
marehemu Sir George Kahama aliyefariki dunia Jumapili akiwa katika Hospitali
ya Taifa Muhimbili jijini Dar es Salaam.
Rais Malinzi amesema taifa limepoteza
mmoja wa watu waliotoa mchango mkubwa katika kupigania maendeleo ya
mpira wa miguu baada ya kupigania Uhuru ambao Watanzania leo wanajivunia
amani.
Pamoja na familia ya marehemu, ndugu,
jamaa na marafiki, Rais Malinzi Dkt Magufuli amewapa pole wanachama
wote wa Chama Cha Mapinduzi, akisema ni kielelezo cha kiongozi aliyetukuka.
“Kabla ya Uhuru Mzee wetu, Mzee
Kahama alikuwa kiongozi shupavu na mzalendo, alama ambayo ametuachia
sisi Watanzania leo hii tunajivunia amani,” alisema Rais Malinzi.
Rais Malinzi ambaye katika vikao
vyake vya jana hapa Dar es Salaam, alikuwa akitoa nafasi ya kumkumbuka
Sir George, akisema msiba huo pia ni wa TFF kwa kuwa mmoja wa watoto
wake, Joseph ni Mjumbe wa Mfuko wa Bodi ya Maendeleo ya Mpira wa Miguu
wa TFF.
Mwenyezi Mungu aipumzishe roho yake
mahali pema peponi, Amina.
EmoticonEmoticon