Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Doto James akizungumza
na Wanahabari kuhusu Wizara yake ilivyotekeleza Agizo la Rais Dkt. John
Magufu kuhusu kumlipa Mkandarasi ayejenga Uwanja wa Ndege wa Kimataifa
wa Julius Nyerere (Terminal 3).
Kwa mujibu wa Katibu Mkuu Doto James, Wizara ya Fedha na Mipango imemlipa
Mkandarasi anayejenga Mradi wa upanuzi wa wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa
wa Julius Nyerere(Terminal 3) Kampuni ya BAM International kiasi cha
Euro Milioni 9.5 sawa na zaidi ya Tsh. Bilioni 22 za Kitanzania mara
baada ya kuhakiki madai hayo.
Katika Hatua nyingine Wizara ya Fedha inaandaa Malipo ya awali (Advance
Payment) kiasi cha Tsh. Bilioni 300 kwa ajili ya kumlipa Mkandarasi
anayejenga Mradi wa Ujenzi wa Reli ya Kisasa ya Kutumia Umeme na Mafuta(Standard
Gauge) katika awamu ya kwanza itakayoanzia kutoka Dar es Salaam hadi
Morogoro katika awamu yake ya kwanza ya Ujenzi huo.
EmoticonEmoticon