KUELEKEA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI,WANAWAKE WATAKIWA KUJIJENGEA TABIA YA KUPIMA AFYA ZAO

February 28, 2017


 Na  Woinde Shizza,Arusha

Wanawake wote hapa nchini wametakiwa kujijengea tabia ya kupima afya zao mara kwa mara ili kuweza kujua matatizo  ya mwili waliyonayo na kuyatatua  kabla ya madhara makubwa kutokea .

Hayo yamebainishwa leo na  mkurugenzi wa kampuni   ya Phide  entertaiment  Phidesia Mwakitalima wakati alipokuwa akiongea na waandishi wa habari juu ya maandalizi ya wiki   wanawake duniani ambayo inatarajia kuanza March mbili ambapo kwa mkoa wa Arusha maadhimisho hayo yanatarajiwa kufanyika kwa muda wa siku  saba katika viwanja vya kumbukumbu  ya sheikh Amri Abeid  .
Alisema kuwa wanawake wengi wamekuwa awana tabia ya kupima afya zao mara kwa mara  kitu ambacho ni hatari mno kwani maisha ya sasa ukilinganisha na hali ya tabia nchi ilivyo pamoja na vyakula ambavyo vinaliwa kwa kipindi hichi.
Alisema kuwa kutokana na tatizo hilo kuonekana hivyo  kampuni ya Phide entertaiment wameamua kuandaa kuandaa maadhimisho haya kwa kuwapa fursa wanawake kujitokeza kupima afya zao bure ambapo alisema  tukio zima litafanyika katika viwanja vya kumbukumbu ya Sheikh Amri Abeid  kwa muda wa siku saba  ambapo alisema kuwa maadhimisho haya yataanza rasmi  March 2 hadi March  nane.
" tamasha hili kubwa linawapa  fursa  wanawake kuweza  kupima Afya yako bure na magonjwa ambayo yatapimwa katika wiki hii ni pamoja na Moyo, Kisukari, Macho, na figo hivyo napenda kuwasihi wanawake wenzangu wote wajitokeze kwa wingi waje wapime afya zao  na wajijue vizuri "alisema Phide

Aidha alisema kuwa mbali  na kupima afya pia wiki hiyo itatumika kwa ajili ya kuwapa wanawake ushauri juu ya kupima afya zao mara kwa mara  ambapo watawapa elimu ya kutosha .

"unajua kipindi hichi wanawake wamekuwa wanapata magonjwa ya haina mbalimbali na wingine wamekuwa wanapuuzia kwenda hospitali kupima afya zao mara kwa mara hivyo tamasha hili la wiki nzima litatumika kuwaelimisha wanawake faida za kupima afya zao mara kwa mara"alisema Phide

Alimalizia kwa kuwataka wanawake wote kutopuuzia wiki hiii kwani ni muhimu sana kwa kujotokeza kupima afya zao na wajue mfumo mzima wa miiili yao ilivyo pamoja na kupata ushauri kutoka kwa wataalamu  wa afya .

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »