Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa
Pili wa Rais – Zanzibar Bw. Joseph Meza (wa kwanza kulia) akiongoza
kikao kazi cha Makatibu Wakuu kutoka Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Katikati ni Mwenyekiti
Mwenza Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Prof. Faustin Kamuzora.
Kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya Muungano kutoka Ofisi ya Makamu wa
Rais Dar es Salaam Bw. Baraka Rajab. Kikao kazi hicho kimefanyika leo
tarehe 05/01/2017 katika Ukumbi wa zamani wa Baraza la Wawakilishi
Zanzibar na kwa pamoja wamejadili changamoto za Muungano.
Baadhi ya Makatibu Wakuu kutoka
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakifuatilia kikao kazi
kilichojadili changamoto za Muungano. Kikao hicho kimefanyika katika
Ukumbi wa zamani wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar.
Baadhi ya Makatibu Wakuu kutoka
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakifuatilia kikao kazi
kilichojadili changamoto za Muungano. Kikao hicho kimefanyika katika
Ukumbi wa zamani wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar.
Bw. Shomari Omar Shomari Naibu
Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji, Bi. Fatma
Gharib Bilal Katibu Mkuu Kazi, Uwezeshaji, Wazee, Vijana, Wanawake na
Watoto na Bi. Khadija Bakari Juma Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo
ya amali kwa pamoja wakifuatilia kikao kazi kilichojadili changamoto za
Muungano na namna bora ya kuzipatia ufumbuzi.
Mwenyekiti na Mwenyekiti Mwenza
Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais – Zanzibar Bw. Joseph Meza
(wa pili kulia) na Prof. Faustin Kamuzora (wa tatu kutoka kulia) wakiwa
katika picha ya pamoja na Makatibu Wakuu kutoka Serikali ya Mapinduzi
Zanzibar na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mara baada ya
kumalizika kwa kikao kazi.
Pichani ni Mwenyekiti na
Mwenyekiti Mwenza Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais – Zanzibar
Bw. Joseph Meza (wa pili kulia) na Prof. Faustin Kamuzora (wa tatu
kutoka kulia) wakiwa katika picha ya pamoja na Sekretarieti iliyoratibu
kikao hicho ikiwa na wajumbe kutoka Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
EmoticonEmoticon