Mkuu wa wilaya ya Tanga,Thobias Mwilapwa akizungumza wakati wa mkutano wa wananchi wa Kijiji cha Marungu ambao ni sehemu ya waathirka na
mgogoro huo sambamba na muwekezaji wa shamba hilo na kusema kuwa makubaliano
yaliyofikiwa baina ya serikali na wafugaji hao lazima yatekelezwe kwa wakati
ili kuepusha vurugu za uvunjifu wa amani uliokuwa ukijitokeza mara kwa mara.
Katibu Tawala wa wilaya ya Tanga(DAS),Faidha Salim akizungumza katika mkutano huo
Diwani wa Kata ya Marungu (CCM) Mohamed Mambea akizungumza wakati wa mkutano huo
Mkuu wa wilaya ya Tanga,Thobias Mwilapwa katikati akiandika baadhi ya maswali ya wananchi ambao walikuwa wakiuliza kwenye mkutano huo.
Wananchi wakifuatilia mkutano wa hadhara wa Mkuu huyo wa wilaya.
MKUU wa
Wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa ameingilia kati mgogoro wa wafugaji na
mwekezaji wa shamba la mkonge la Marungu Mkoani Tanga na kutoa miezi mitatu kwa
wafugaji hao kuhakikisha wanaondoka katika shamba hilo kabla ya serikali haijatumia
nguvu ya kuwahamisha.
Akizungumza
katika kikao cha wananchi wa Kijiji cha Marungu ambao ni sehemu ya waathirka na
mgogoro huo sambamba na muwekezaji wa shamba hilo na kusema kuwa makubaliano
yaliyofikiwa baina ya serikali na wafugaji hao lazima yatekelezwe kwa wakati
ili kuepusha vurugu za uvunjifu wa amani uliokuwa ukijitokeza mara kwa mara.
Maamuzi
hayo yamekuja ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa agizo lililotolewa siku chache
zilizopita na Mh;WAziri MKuu la kuwataka Wakuu wote wa Wilaya nchi nzima kuhakikisha
wanamaliza migogoro ya ardhi iliyondani ya uwezo wao ili kutoa fursa kwa
wananchi kuendelea na shughuli zao.
Mwilapwa
alisema kumekuwepo na madhara mengi yanayojiketokeza kutokana na kuwepo kwa
migogoro ya wakulima na wafugaji hadi kufikia kutokea mapigano yanayohatarisha
amani iliyopo baina ya makundi hayo mawili jambo ambalo serikali imejidhatiti
kumaliza migogoro hiyo kwa makubaliano ya mazungumzo.
“Kumekuwepo
na mapigano ya mara kwa mara baina ya wakulima,mwekezaji na wafugaji jambo linalovunja
amani na hata kuhatarisha maisha ya watu nisema ikiwa makubaliano haya
hayatatekelezwa basi Serikali itaingilia kati na itawahamisha wafugaji hao kwa
nguvu”Alisema Mwilapa.
Kwa
upande wa Diwani wa kata ya Marungu Mohamed Mwambea alisema kuwepo kwa wafugaji
hao katika shamba hilo ndani Kijiji hicho kumeleta madhara makubwa kutokana na
kutokea mapigano kwa pande hizo mbili na
kutokea uharibifu wa mazao ya wananchi wanaojishughulisha na kilimo Kijijini
hapo.
Mwambea
alisema imekuwa kawaida kwa wafugaji kushinda katika kesi zao dhidi ya wakulima
jambo linaloshangaza wanapata wapi haki ya kuweza kushinda kila aina ya kesi
zinazojitokeza baina ya wakulima na wafugaji.
“Ifike
wakati kwa Serikali iwe inatenda haki kwa wakulima dhidi ya wafugaji ili
kujenga usawa kwa jamii hizo mbili ambazo zinaingia katika migogoro
inayohatarisha maisha yao na hata jamii inayotuzunguka”Aalisema Mwambea.
Nae Meneja
wa shamba la mkonge la Marungu Casmir Joackim alisema wameshindwa kuendelea na
uzalishaji katika shamba hilo kwa zaidi ya miaka miwili kutokana kuingiliwa na
wafugaji hao waliohamishia shughuli zao za kifugaji na makazi katika shamba
hilo.
Joackim
alisema dhamira ya muwekezaji wa shamba hilo ni kutekeleza agizo la Serikali ya
awamu ya tano ya kuwataka wawekezaji wote nchini wayaendeleze mashamba yao
kiuzalishaji na hata kutoa ajira kwa wananchi ili kukwepa mkono wa Serikali
unaoweza kufuta hati ya umili wa shamba hilo na kurudishwa serikalini kwa ajili
ya kugawiwa upya wananchi.
“Ikiwa
ndani ya shamba letu wapo wafugaji wanaendelea na shughuli zao za ufugaji
pamoja na maisha kwa ujumla tangu mwaka 2014 ni namna gani tunaweza kundeleza
shughuli zetu,huoni mkono wa Serikali unaweza kutukumba lazima tutendewe haki
kwa hawa watu ambao ni wavamizi”Alisema Joackim.
EmoticonEmoticon