WANAWAKE NA MAENDELEO FOUNDATION
D A R ES SALAAM | IJUMAA |DESEMBA
2, 2016
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Katika
gazeti la Raia Mwema toleo No 486 la Tarehe 30 Novemba, 2016 kumeandikwa habari
yenye kichwa kilichosomeka “Mali za Salma Kikwete kuuzwa kwa mnada?”. Katika habari hiyo kumetolewa madai ati kwamba
taasisi ya WAMA inayoongozwa na Mheshimiwa Mama Salma Kikwete inao mzigo mkubwa
bandarini ambao haujalipiwa ushuru na kodi. Na kwa sababu hiyo, Mamlaka ya
Mapato Tanzania imepanga kuuza mali hizo.
Kwa
niaba ya Taasisi ya WAMA napenda kutoa masikitiko yetu kwamba habari hizo ni za
uongo na hazina ukweli wowote. Kwa maoni yetu gazeti hilo lina dhamira mbaya dhidi
ya Taasisi ya WAMA na Mwenyekiti wake, Mheshimiwa Mama Salma Kikwete. Nia yao
ni kupaka matope na kuchafua majina na sifa ya taasisi yetu na kiongozi wake.
Ukweli
kuhusu jambo hili ni kwamba, WAMA ilitumiwa maboksi Kumi na Moja (11) ya vitabu
vikiwa ni zawadi (grant) kutoka Nakayama Foundation ya Japani ambayo ndiyo iliyofadhili
ujenzi wa Shule ya Sekondari ya WAMA-Nakayama iliyopo Nyamisati, Kibiti. Maboksi
hayo yaliyotumwa kupitia BL 243016002211 yaliwasili bandarini tarehe 27/06/2016.
Yalitolewa tarehe 10/8/2016 baada ya WAMA kulipia kodi zote na ushuru wote unaotahili
tarehe 26/07/2016.
Vitabu hivyo
vimekwishapelekwa shuleni na wanafunzi wanavitumia. Hakuna mzigo wowote wa
Taasisi ya WAMA uliopo bandarini unaosubiri kutolewa wala kuuzwa na TRA. Hivyo
basi, gazeti hilo kuandika kuwepo kwa mzigo mkubwa wa WAMA bandarini ni jambo
la kughushi ambalo limefanywa kwa dhamira mbaya na kwa sababu wanazozijua wao.
Tumelitaka
gazeti la Raia Mwema limuombe radhi Mwenyekiti wa WAMA Mheshimiwa Mama Salma
Kikwete na kuiomba radhi WAMA Foundation kwa kuandika taarifa za uongo. Gazeti hilo
limechafua sifa ya Mwenyekiti wa WAMA na WAMA Foundation kiasi ambacho wanao
wajibu wa kuomba radhi na kusafisha majina na heshima zetu mbele ya jamii.
Ikiwa hawatatekeleza
haya ndani ya kipindi cha siku Saba, yaani kabla ya tarehe 07 Desemba, 2016, tutalazimika
kuchukua hatua zipasazo za kisheria.
Daudi
Nasib,
Katibu
Mtendaji,
Dar es
Salaam,
Tel:
+255 22 2781287
info@wamafoundation.or.tz
EmoticonEmoticon