Waziri wa
Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. January Makamba akizungumza
na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Kebwe Stephen Kebwe. Waziri Makamba yuko
Mkoani Morogoro kwa ziara ya kikazi ya siku mbili.
Waziri wa
Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. January Makamba, wa
tatu kutoka kulia akiangalia chanzo cha maji kilichovamiwa katika Mto Mambogo
Wananchi wa Kijiji cha Parakuyo
wakisalimiana na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira)
Mhe. January Makamba kabla ya kufanya mkutano wa hadhara kijijini hapo.
Sehemu ya
Wananchi wa waliojitokeza katika Mkutano wa hadhara katika kijiji cha Parakuyo
Wilayani Kilosa. Wananchi hao walimweleza Waziri changamoto
zinazowakabili juu ya Hifadhi ya mazingira
Sehemu ya Wananchi wa waliojitokeza katika Mkutano wa hadhara katika kijiji cha Parakuyo Wilayani Kilosa.
Na Lulu
Mussa ,Morogoro
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. January Makamba
ameitaka jamii ya watu wa Parakuyo katika Wilaya ya Kilosa kuishi kwa amani,
uvumilivu na upendo miongoni mwao kwani ndio misingi ya watanzania.
Rai
hiyo imetolewa leo katika Mkutano wa hadhara uliojumuisha jamii za wakulima na
wafugaji ambazo zimekuwa na migogoro ya mara kwa mara. Waziri Makamba alizitaka
jamii hizo kuishi kwa amani na kuhifadhi mazingira kwa faida ya sasa na vizazi
vijavyo.
Miongoni
mwa changamoto zilizobainishwa na jamii hiyo ni kutokuwa na elimu juu ya
mabadiliko ya Tabianchi na athari zake pamoja na kutokuwepo na matumizi bora ya
ardhi.
Waziri
Makamba ameuagiza uongozi wa Wilaya na Kijiji kushirikiana pamoja kuunda kamati
ya 'Amani' itakayokuwa na wajumbe kutoka pande zote mbili za wakulima na
wafugaji na viongozi wa madhehebu ya dini ili kutafuta suluhu ya kudumu baina
ya pande mbili ambazo zimekua na migogoro ya mara kwa mara. "Undeni Kamati
hii mapema na Ofisi yangu itagharamia mafunzo kwa Kamati husika juu ya namna
bora ya kutatua migogoro" alisisitiza Waziri Makamba.
katika
jitihada za kukuza uelewa wa masuala ya mazingira na changamoto zake, Waziri
Makamba ameitaka Serikali ya Kijiji kuunda Kamati ndogondogo za Mazingira ambazo
zipo kwa mujibu wa sheria ya Mazingira na kuahidi kuipati mafunzo Kamati hizo
ikiwa ni pamoja na kutengeneza sheria ndogo ndogo zitakazotumika kama nyenzo ya
kuhifadhi na kusimamia Mazingira ya maeneo yao.
Aidha,
Waziri Makamba amesema kuwa mpango wa matumizi bora ya ardhi ni muhimu sana na
kuitaka jamii ya Parakuyo na Twa twa twa kushiriki kikamilifu katika zoezi la
kuhakiki na kuhesabu mifugo yako ili kubaini ni ardhi kiasi gani inahitajika
kwa wakulima na kiasi gani kwa wafugaji. "ndugu zangu niwasihi, Serikali
ina nia ya dhati ya kuhakikisha kuna kuwa na matumizi bora ya ardhi, hivyo
nawashauri mmshiriki kikamilifu katika zoezi hilo ili kupata uwiano wa idadi ya
mifugo na ardhi iliyopo" Makamba aliongezea.
Awali
katika ziara ya kikazi ya siku mbili Mkoani Morogoro Waziri Makamba pia
alitembelea chanzo cha maji na kujionea changamoto za kimazingira katika mto
Mambogo.






EmoticonEmoticon