MD KAYOMBO ABAINI UBADHILIFU WA MAPATO KATIKA DUKA LA DAWA HOSPITALI YA SINZA

October 08, 2016
 Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo alipotembelea wodi ya wanawake
Watumishi, wauguzi na madaktari wakimsikiliza kwa makini Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo alipozuri katika hospitali ya Manispaa ya Ubungo kwa ziara ya kikazi
Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo akiwasili Ofisi za Manispaa ya Ubungo

Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo Akitoa maelekezo wakati akikagua ufanisi wa kazi katika Hospitali ya Manispaa ya Ubungo
Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo akisikiliza kwa makini maelezo ya jinsi wanawake wanavyohudumiwa katika wodi ya wanawake

Na Mathias Canal, Dar es salaam

Duka la Dawa za Binadamu lililopo katika Hospitali ya Manispaa ya Ubungo iliyopo katika Mtaa wa Sinza Jijini Dar es salaam limekutikana na unadhilifu wa fedha za Umma kinyume na utaratibu wa matumizi ya fedha hizo.

Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo ameyabaini hayo baada ya kukagua mapato na matumizi ya Duka hilo na kugundua uwapo wa ubadhilifu huo mdogo mdogo ambao ameahidi kutuma mkaguzi wa ndani ili kukagua hesabu za duka hilo.

MD Kayombo amebainisha hayo wakati wa kikao cha kazi na watumishi wa Hospitali hiyo mara baada ya kuzuru na kuwa na kikao cha pamoja ili kukumbushana majukumu ya kazi ikiwa ni pamoja na kujitambulisha ili kisikiliza kero za watumishi hao na kuzitafutia ufumbuzi.

Kayombo amebaini kuwa Duka hilo la Dawa za binadamu katika Hospitali ya Manispaa ya Ubungo lina Account mbili zilizofunguliwa kwa ajili ya matunzo ya fedha za mauzo jambo ambalo sio sahihi kisheria katika Taasisi moja ya serikali kuwa na Account mbili za Bank.

MD Kayombo ameahidi kubadilisha Mfumo wa kukusanya Mapato katika Hospitali hiyo kuhamia mfumo wa kisasa ili Serikali iweze kukusanya fedha za kutosha ambapo mfumo wa sasa mapato mengi yanapotea kwani kufanya hivyo itarahisisha Hospitali hiyo kuweza kujisimamia katika maswala ya matumizi madogo madogo na kuweza kuongeza uwezo wa kunua dawa za kutosha kwa mahitaji husika.

Kuhusu kutoa na kupokea Rushwa MD Kayombo amesema kuwa hakuna asiyetambua kuwa jambo hili linawanyima haki wananchi wengi wanyonge hivyo watumishi wote katika Hospitali hiyo wameonywa kujihusisha na kadhia hiyo kwani endapo mtumishi yeyote atabainika kufanya hivyo atachukuliwa hatua haraka iwezekanavyo ili kuwa fundisho kwa wengine.

"Watumishi wote mnatakiwa kuwa Clean Officials katika mazingira ya kazi hivyo ni lazima kujiepusha na ubadhilifu wa fedha za Umma kwani kila mmoja anapaswa kuridhika na kipato anachopata, Pia nawaahidi kila mmoja kumpatia Extra Duty Allowance kulingana na Bajeti ya mwaka wa fedha 2016/2017.

MD Kayombo ametembelea Wodi zote Hospitalini hapo na kujionea hali halisi ya utoaji huduma ambapo pia ametembelea Ofisi zote zinazotoa huduma na kukutana na wataalamu mbalimbali ambapo wameelezea changamoto zao jambo ambalo Mkurugenzi huyo ameahidi kulifanyia kazi haraka iwezekanavyo kwani lipo ndani ya uwezo wake.

Md Kayombo Amewaonya Wakuu wa Idara kuacha tabia ya kuwanyanyasa na kuwagawa watumishi katika sehemu za kazi ili kuongeza ufanisi katika utendaji kazi katika kuwahudumia wananchi.

Kwa upande wao baadhi ya watumishi katika Hospitali hiyo wamempongeza Mkurugenzi huyo wa Manispaa ya Ubungo kwa ziara yake katika Hospitali hiyo kwani amekuwa Mkurugenzi wa kwanza kuzuru Hospitalini hapo na kujionea hali halisi ya utoaji huduma na sio kusimuliwa.

MD Kayombo ametoa namba ya simu kwa ajili ya matumizi ya dharura kwa watumishi hao ili waweze kuripoti matukio ya haraka ambayo yanakuwa nje ya uwezo wao.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »