OFISI YA MAKAMU WA RAIS
TANGAZO KWA UMMA
UZUIAJI WA UTUPAJI
OVYO USIO WA KITAALAMU WA TAKA ZA
MAHOSPITALI.
Sheria ya usimamizi wa
Mazingira ya mwaka 2004 inapiga marufuku
uchafuzi wa mazingira ikiwa ni pamoja na unaotokana na taka za mahospitali. Aidha Kanuni za Taka Hatarishi za mwaka 2009, zinasisitiza utenganishi wa taka mbali mbali zitokazo kwenye mahispotitali kwa kuzitibu
katika namna ambayo haitaleta athari katika mazingira na afya ya binadamu. Pia
Kanuni zinahimiza matumizi ya teknologia sahihi kama vile matumizi ya incinerators
ambazo huchoma taka za mahospitali na kuziteketeza
kabisa.
Ofisi yangu imefuatilia na kugundua
kuwa taka nyingi za mahopitali, taka kutoka katika maduka ya madawa zilizoisha muda wake zinatupwa
ovyo au kuharibiwa kwa utaratibu usio kubalika
kitalaamu. Tumefuatalia na kukuta malundo ya madawa chakavu na vifaa vya
hospitali vilivyotumika katika maeneo
ya visiwa vya Bongoyo na Mbudya. Aidha madawa chakavu yanatumpwa holela katika
dampo la Pungu Kinyamwezi. Hii ni hatari
sana kwa mazingira na kwa afya ya binadamu.
Kuanzia sasa ni marufuku kutupa
taka hizi katika utaratibu usio wa kawaida. Kila hospitali na zahanati au kituo cha afya kihahakikishe kinatumia
incinerators au utaratibu mwingine ulio
sahihi kwa mujibu wa sheria ya mazingira na kanuni zake. Aidha ninaiagiza NEMC
kuanzia sasa wafanye msako mkali kubaini mahospitali na watu wanaokiuka agizo
hili. Nimewapa mwezi mmoja na kwa wale wanaofanya hivyo waache mara moja. Kwa msako huu atakayebainika kukiuka hatua
kali za kisheria zinachukuliwa dhidi yake.
Nichukue fursa hii kutoa tena pole kwa wezentu wa Mkoa wa Kagera na
maeneo ya jirani kwa athari za tetemeko la ardhi.
Baada ya tatetemeko kuna athari kubwa za kimazingira ambazo zimejitokeza. Hivyo mimi binafsi
ninafuatilia suala hili kwa ukaribu na kuhakikisha athari ambazo zimejotokeza na zinazoendelea
kujitokeza zinashughulikiwa kwa haraka.
Nimeagiza Ofisi yangu pamoja na NEMC washirikiane kwa ukaribu sana na
watendaji wa Mkoa na Kamati mbalimbali zilizoundwa kushughulikia maafa haya na
kufanya tathmini ya athari za mazingira zilizojitokeza na
kuelekeza hatua za haraka kuchukuliwa ilikupunguza madhara kwa mazingira na
binadamu.
Pia, napenda kutumia fursa hii kuukumbusha
umma juu ya dhamira ya Serikali ya
kupiga marufuku matumizi ya mifuko na vifungashio vya ya plastiki ifikapo
Januari Mosi 2017.
Adhma ya Serikali ya kupiga marufuku matumizi ya mifuko na vifungashio vya plastiki ni kuepusha athari
za kiafya na mazingira zinazoendelea kujitokeza kutokana na matumizi ya mifuko
hiyo. Hivyo basi wazalishaji, waagizaji, wasambazaji, wauzaji na watumiaji wa mifuko hiyo wanakumbushwa kuendelea na zoezi
la kuondosha pamoja na kusitisha uzalishaji wa mifuko hii.
IMETOLEWA NA
JANUARY Y. MAKAMBA (MB.)
WAZIRI WA NCHI OFISI
YAMAKAMU WA RAIS
MUUNGANO NA MAZINGIRA
21/9/2016
EmoticonEmoticon