MAMA SAMIA |
Ofisi
ya Makamu wa Rais imekanusha vikali kuwa taarifa inayosambazwa kwenye
baadhi ya mitandao kuwa Makamu wa Rais, Mama Samia Suluhu Hassan ameomba
kujiuzulu wadhifa wake, ni ya uongo.
Taarifa
ilyotolewa hivi punde leo, na Ofisi ya Makamu wa Rais, imesema, taarifa
hiyo ni ya uzushi na uongo na kuomba wananchi kuipuuza mara moja kwa
kuwa mbali ya kupotosha wananchi lakini pia ina lengo la uchochezi na
kuliweka taifa kwenye taharuki.
"Taarifa
hiyo ni ya uchochezi inayolenga kuliweka Taifa kwenye taharuki. Mhe.
Makamu wa Rais yuko bega kwa bega na Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania katika kufanya kazi zao kwa mujibu wa Katiba ya nchi ili
kuwaletea wananchi maendeleo", imesema sehemu ya Taarifa hiyo na
kuongeza;-
"Ofisi
ya Makamu wa Rais inawataka wananchi na Watanzania kwa ujumla kupuuza
taarifa hiyo ambayo inalenga kupotosha umma kuhusu ushirikiano mzuri
uliopo baina ya Viongozi wetu".