Na Mwandishi Wetu, Bumbuli
KUTOKANA na kukosa umeme katika ofisi za Halmashauri ya
Bumbuli, Taasisi ya kifedha ya Bayport Financial Services, imemkabidhi jenereta
Mkurugenzi wa halmashauri hiyo ili waweze kufanya kazi zao kwa ufanisi na
kufanikisha maendeleo kwa wakazi na wananchi wa Bumbuli, mkoani Tanga.
Meneja wa Bayport Financial Services, Kanda ya Kaskazini, Emmanuel Nzutu, kulia, akipeana mikono na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Bumbuli, Peter Nyalali kushoto baada ya kumkabidhi msaada wa jenereta kutoka kwenye taasisi yao ya Bayport kwa ajili ya ofisi ya Halmashauri ya Bumbuli ili iweze kujiendesha vizuri kutokana na ukosefu wa umeme kwenye majengo yao ya ofisi. Nyuma ya Nzutu ni Meneja wa Bayport wilaya ya Lushoto Consolata Thomas, akifuatiwa na Afisa Utumishi wa Bumbuli, Fatma Mrope. Picha na Mpiga picha wetu Bumbuli.Makabidhiano hayo yamefanyika mwishoni mwa wiki iliyopita yakiongozwa na Meneja wa Bayport Kanda ya Kaskazini, Emmanuel Nzutu, Meneja wa Bayport, wilayani Lushoto mkoani Tanga, Consolata Thomas, Mkurugenzi Mtendaji Bumbuli Peter Nyalali, Afisa Utumishi wa Bumbuli Fatma Mrope na baadhi ya watumishi wengine wa halmashauri hiyo.
Meneja wa Bayport Financial Services, Kanda ya Kaskazini, Emmanuel Nzutu, kulia, akiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Bumbuli, Peter Nyalali kushoto baada ya kumkabidhi msaada wa jenereta kutoka kwenye taasisi yao ya Bayport kwa ajili ya ofisi ya Halmashauri ya Bumbuli ili iweze kujiendesha vizuri kutokana na ukosefu wa umeme kwenye majengo yao ya ofisi. Nyuma ya Nzutu ni Meneja wa Bayport wilaya ya Lushoto Consolata Thomas, akifuatiwa na Afisa Utumishi wa Bumbuli, Fatma Mrope. Picha na Mpiga picha wetu Bumbuli.
Mwandishi wa Star Tv mkoani Tanga, Mbonea Herman akiwajibika katika tukio la Bayport Financial Services kukabidhi jenereta kwa ofisi ya Halmashauri ya Bumbuli, mwishoni mwa wiki.
Akizungumza katika makabidhiano hayo, Meneja wa Bayport
Kanda ya Kusini, Nzutu, alisema kwamba taasisi yao imeona ikabidhi msaada wa
jenereta kwa mkurugenzi wa Bumbuli ili watumishi kwenye ofisi hiyo watoe huduma
bora na kwa wakati ili kuharakisha maendeleo katika serikali ya Hapa Kazi Tu,
inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dr John
Pombe Magufuli.
“Bayport ni taasisi inayotoa huduma za mikopo huku tukifanya
kazi kwa karibu na watumishi wengi nchini Tanzania, hivyo baada ya kuona ofisi
za Halmashauri Bumbuli hazina umeme na wafanyakazi wanapata tabu, tukaona tuje
kuwakomboa kwa kuwapa jenereta.
“Tunaamini sasa wana Bumbuli watahudumiwa vizuri na kwa
wakati, maana awali mtu anaweza kukosa huduma pale inapohitaji kifaa
kinachoendeshwa na umeme, hivyo Bayport tunaamini tutaendelea kufanya kazi kwa
karibu na kushirikiana na viongozi wote ili kuhakikisha kwamba nchi yetu
inasonga mbele,” Alisema.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo ya Bumbuli,
Nyalali, aliwashukuru Bayport Financial Services kwa kuwakomboa baada ya kuwapa
msaada wa jenereta litakalowezesha utoaji huduma bora pamoja na ukusanyaji wa
mapato na rekodi kwa ofisi muhimu za halmashauri yao.
“Kukosekana umeme kwa ofisi nyeti za halmashauri ni jambo
linaloweza kuwafanya watumishi wafanye kazi chini ya kiwango pamoja na
kushindwa kukusanya mapato ya serikali kwa wakati kwa sababu kuna vifaa ili
vijiendeshe lazima umeme uwepo,” Alisema Mkurugenzi huyo ambaye ameripoti
kazini kwa mara ya kwanza tangu alipoteuliwa kuongoza halmashauri hiyo.
Afisa Utumishi wa Bumbuli, Fatma Mrope aliwashukuru Bayport
huku akisema kupata jenereta kutawafanya watumishi wote wakose visingizio vya
umeme hivyo kufanya kazi kwa nguvu zote za kuwatumikia wana Bumbuli na
Watanzania kwa ujumla.
“Ofisi za Halmashauri yetu ya Bumbuli ilikuwa na changamoto
kubwa ya kukosa umeme, hivyo ingawa tunaendelea na juhudi za kupata umeme kutoka
Mamlaka ya Umeme Vijijini (REA), tunafurahia sana msaada huu kutoka kwa watu wa
Bayport, maana utakuwa mkombozi kwa kiasi kikubwa mno kwa sababu nikiwa kama
Afisa Utumishi naifahamu adha tuliyokuwa tunaipata,” alisema Fatma.
Mbali na kutoa mikopo ya fedha taslimu, Bayport pia inatoa
huduma ya mikopo ya viwanja katika maeneo mbalimbali kama vile Kibaha,
Chalinze, Bagamoyo, Kigamboni na Kilwa, huku ikifanikiwa kuwa na ofisi katika
mikoa yote ya Tanzania Bara na wilaya mbalimbali kwa ajili ya kusogeza huduma
zao karibu na wananchi.
EmoticonEmoticon