Chama cha
Wamiliki/Waendeshaji wa Mitandao ya Kijamii nchini 'Tanzania Bloggers Network'
(TBN) kinasikitishwa na kulaani vitendo vya baadhi ya Vyombo vya Habari kutumia
kazi za wanachama wake (picha, video, habari) bila idhini na bila kutoa maelezo
stahiki ya vyanzo vya kazi hizo.
Mfano mmoja
ni Gazeti la kila siku la Majira, toleo namba 8217 la Alhamisi Julai 7, 2016
ambalo bila aibu lilichukua picha katika Mtandao wa Michuzi Blog ina kuitumia
pamoja na malezo yake bila ridhaa wala kutoa
kueleza chanzo cha hiyo picha.
Vile vile
Wahariri wa Majira kwa makusudi waliondoa alama maalum ya kumbukumbu iliyowekwa
katika picha hiyo (watermark-logo) na kuichapisha katika ukurasa wa mbele wa
gazeti hilo, bila kutaja chanzo chake, jambo ambalo ni ukiukwaji wa Sheria na
kinyume na taaluma ya habari.
Kitendo
hicho ambacho pia kimekuwa kikifanywa na baadhi ya magazeti hapa nchini
kimeonesha dhahiri ni jinsi gani baadhi ya vyombo vyenye tabia hiyo
visivyothamini kazi za ‘bloggers’ na mchango wake kwenye tasnia nzima, huku
wakiendelea kulea waandishi na wapiga picha wavivu na wazembe wanaotumia blogs
kama njia ya mkato kupata material.
TBN
inatambua wazi si vibaya vyombo vya habari kutegemeana/kushirikiana kwa kutumia
kazi za chombo kingine lakini ni vema chombo kinachotumia kazi ya mtu mwingine
kumtambua kwa kumtaja katika kazi hiyo ama kukubaliana na chombo husika kabla
ya kufanya hivyo.
Chama cha
Wamiliki/Waendeshaji wa Mitandao ya Kijamii nchini hakitafumba macho kuona kazi
za wanachama wake zikitumiwa na vyombo vingine vya habari bila utaratibu na
wala makubaliano ya kabla kwa wahusika.
Imetolewa na:-
Kamati ya Uongozi TBN Taifa,
Tarehe: 11/07/2016,
Dar es Salaam.
--
______________________________ ______________________________ _______________________
Joachim Mushi, Mwenyekiti wa Tanzania Bloggers Network (TBN) na Mhariri Mkuu wa Thehabari.com.
Mobile:- 0717
030066 / 0756 469470
Web:- www.thehabari.com
EmoticonEmoticon