Meneja wa Benki ya NMB Tawi la Ubungo, Evelyne Mushi (kushoto)
akimkabidhi baba wa watoto pacha wanee, Abednego Andrew Mafuluka mkazi
wa Kimara Mwisho, Dar es Salaam mfano wa hundi ya shilingi milioni 10
ikiwa ni msaada kwa mapacha hao wanne. Benki ya NMB imewafungulia
akaunti za watoto kwa kila mtoto na kuwawekea shilingi cha shilingi
milioni 10, kuwasaidia wazazi na watoto hao hapo baadaye. Wa pili kulia
ni mama mzazi wa mapacha hao, Sara Dimosso akiwa kabeba watoto wake huku
akisaidiwa na nduguye.
Meneja wa Benki ya NMB Tawi la Ubungo, Evelyne Mushi (kushoto)
akimkabidhi mama mzazi wa watoto wanne mapacha, Sara Dimosso (kulia)
mfano wa hundi ya shilingi milioni 10 ikiwa ni msaada kwa watoto mapacha
wanne aliojifungua hivi karibuni. Benki ya NMB imewafungulia akaunti za
watoto kwa kila mtoto na kuwawekea shilingi milioni 10 ikiwa ni
kuwasaidia wazazi na watoto hao hapo baadaye. Katikati ni baba wa watoto
pacha wanee, Abednego Andrew Mafuluka akishiriki kupokea msaada huo.
Mama mzazi wa watoto mapacha wanne, Sara Dimosso (kulia) pamoja na mume
wake, Abednego Andrew Mafuluka (katikati) wakipiga picha ya pamoja na
mfano wa hundi ya shilingi milioni 10 iliyokabidhiwa na Benki ya NMB
ikiwa ni msaada kwa watoto mapacha wanne aliojifungua hivi karibuni.
Kulia ni Meneja wa Benki ya NMB Tawi la Ubungo, Evelyne Mushi mara baada
ya kuwakabidhi, Benki ya NMB imewafungulia akaunti za watoto kwa kila
mtoto na kuwawekea shilingi milioni 10 ikiwa ni kuwasaidia wazazi na
watoto hao hapo baadaye.
Baadhi ya maofisa wa Benki ya NMB wakiwa katika picha na familia ya
Bwana na Bibi Abednego Andrew Mafuluka pamoja na watoto wao mapacha
wanne mara baada ya kukabidhiwa mfano wa hundi ya msaada.
Bwana Abednego Andrew Mafuluka (katikati) akizungumza kuishukuru Benki
ya NMB baada ya kuguswa na kuamua kuwasaidia watoto wao mapacha wanne.
Meneja wa Benki ya NMB Tawi la Ubungo, Evelyne Mushi (kushoto)
akizungumza kuelezea namna Benki ya NMB ilivyoguswa na kuamua kuwasaidia
watoto hao mapacha wanne waliozaliwa pamoja.
Mama mzazi wa watoto mapacha wanne, Sara Dimosso (kulia) pamoja na mume
wake, Abednego Andrew Mafuluka akizungumza kuishukuru Benki ya NMB kwa
kuwasaidia shilingi milioni 10 iwawezeshe katika malezi ya watoto hao.
Baadhi ya maofisa wa Benki ya NMB wakiwa katika picha na familia ya
Bwana na Bibi Abednego Andrew Mafuluka pamoja na watoto wao mapacha
wanne mara baada ya kukabidhiwa mfano wa hundi ya msaada.
EmoticonEmoticon