BAADA YA KUSHINDA RUFAA DHIDI YA ABAJALO FC, TIMU YA PAMBA YA JIJINI MWANZA YAELEZEA MIKAKATI YAKE.

July 16, 2016
Msemaji wa Pamba, Gervas Mbaya (kushoto), akiteta na Slyvester Joseph-VesterJtz @BMG (kulia).
Na BMG

Baada ya jana timu ya soka ya Pamba ya Jijini Mwanza, kupata nafasi ya kucheza ligi daraja la kwanza kutokana na timu ya Abajalo Fc ya Jijini Dar es salaam kupoteza pointi sita kwa kosa la kumchezesha mchezaji wa Kagera Sugar katika michuano ya ligi daraja la pili, timu hiyo imeeleza furaha yake sambamba na mikakati iliyopo katika kuelekea michuano ya ligi daraja la kwanza.

Akibonga na VesterJtz wa BMG, Msemaji wa timu ya Pamba, Gervas Mbaya, amesema wamepokea maamuzi yaliyotolewa na TFF kwa shangwe kubwa baada ya kushinda rufaa waliyokuwa wameikata wakilalamikia ushindi wa timu ya Abajalo Fc.

Amesema ndani ya siku mbili zijazo, uongozi wa timu hiyo utakutana ili kupanga mikakati ni lini timu ya Pamba ianze kufanya mchakato wa usajili ili timu iingie kambini kwa ajili ya maandalizi ya mapema kuelekea michuano ya ligi daraja la kwanza.
Msemaji wa Pamba, Gervas Mbaya (kushoto), akiteta na Slyvester Joseph-VesterJtz @BMG (kulia).

Itakumbukwa kwamba timu ya Pamba SC ya Mwanza na The Mighty Elephant ya Songea zilikata rufaa TFF kuilalamikia timu ya Abajalo FC kwa kumtumia mchezaji wa Kaliua City ya Tabora, Laurence Mugia, wa Kagera Sugar katika michezo ya mtoano wa Ligi daraja la pili kwa ajili ya kupanda daraja la kwanza ambapo baada ya kushinda rufaa hiyo timu zote zilijinyakulia pointi tatu na magoli matatu huku Abajalo ikipoteza pointi sita na hivyo kupoteza nafasi ya kucheza ligi daraja la kwanza.
Bonyeza HAPA Kusikiliza Zaidi. Au Bonyeza Play Hapa Chini.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »