Mbunge
wa Jimbo la Ubungo Mh. Saed Kubenea akisaidiwa kujaza fomu za maombi za
Vitambulisho vya taifa na Afisa Usajili Bi. Hadija Bauji.
Mh.
Saed Kubenea akisaidiwa na Afisa Usajili Bw. Surera kuchukua alama za
vidole wakati wa hatua ya uchukuaji alama za kibaiolojia.
Dr. Harrison Mwakyembe (Mb) akisaidiwa kujaza fomu na Meneja Usajili Vitambulisho vya Taifa, Bi. Julian Mafuru
…………………………………………………………………………………………..
Mamlaka ya Vitambulisho vya
Taifa(NIDA), imeanza kusajili Waheshimiwa Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania; wakati wakiendelea na kikao cha Bajeti
Katika Usajili huo NIDA
inategemea kusajili wabunge wote ambao hawakuwahi kusajiliwa awali na
kupata vitambulisho vya Taifa, pamoja na kugawa vitambulisho
Wabunge wameonyesha mwamko mkubwa
katika kutumia fursa hii adhimu, kwa kuhakikisha kwamba wanakuwa mstari
wa mbele kutimiza haki yao ya kikatiba ya kusajiliwa na kupata
kitambulisho cha Taifa; ambacho kimekuwa na faida nyingi kiuchumi,
kijamii na kisiasa
Mpaka sasa NIDA imeshatoa zaidi
ya vitambulisho zaidi ya milioni 2.5 na kwa sasa NIDA iko mbioni kuanza
usajili kwa kutumia mtaji wa taarifa toka NEC ambapo zaidi ya wananchi
milioni 22 watasajiliwa na kupewa namba ya utambulisho ili kuanza
matumizi mbalimbali
EmoticonEmoticon