Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na
Mipango Dkt. Servacius Likwelile (kushoto) akiongea na waandishi wa
habari leo jijini Dar es salaam ambapo amesema kuwa wizara hiyo
imeendelea kufanya vizuri katika ukusanyaji wa mapato na katika kipindi
cha mwezi Februari mwaka huu zimekusanywa zaidi ya Sh. trilioni 1
tofauti na mwanzo ambapo zilikuwa zkikusanywa Sh.bil 850. Kulia ni
Katibu Mkuu Wizara ya Waziri wa Afya, Maendeleo, Jinsia, Watoto na Wazee
Mpoki Ulusubisya.
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya
Mapato Tanzania (TRA) Alphayo Kidata akifafanua kwa waandishi wa habari
leo jijini Dar es salaam jinsi Mamlaka hiyo ilivyofanikiwa kukusanya
mapato kutoka trilioni 1.2 kwa mwezi Disemba mpaka trilioni 1 na bilioni
79 kwa mwezi Januari na kwa mwezi Februari wanatarajia kukusanya
trilioni 1.013 na tayari wamefikia nusu ya malengo waliyojiwekea.
Katibu Mkuu Wizara ya Elimu,
Sayansi,Teknologia na Ufundi Tarishi Kibenga amesema Wizara yake
itazitumia fedha walizopewa mwezi huu kulingana na malengo
yaliyokusudiwa ikiwemo fedha za mafunzo kwa vitendo kwa wanafunzi wa
Diploma na wanafunzi wa chuo kikuu. Wa kwanza kushoto ni Kamishna Mkuu
wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Alphayo Kidata.
Katibu Mkuu Wizara ya Waziri wa
Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Watoto na Wazee akifafanua namna
Wizara yake ilivyojipanga kuzitumia fedha walizopata mwezi huu ambapo
amesema zitatumika kulingana na malengo yaliyokusudiwa ikiwemo fedha za
mradi wa ujenzi wa Chuo cha Tiba cha Kimataifa cha Muhimbili eneo la
Mloganzila nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam.
Baadhi ya Waandishi wa habari
wakimsikiliza Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Servacius
Likwelile akiongea na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam
ambapo amesema kuwa wizara hiyo imeendelea kufanya vizuri katika
ukusanyaji wa mapato na katika kipindi cha mwezi Februari mwaka huu
zimekusanywa zaidi ya Sh. trilioni 1 tofauti na mwanzo ambapo zilikuwa
zkikusanywa Sh.bil 850.
(Picha na Eleuteri Mangi- MAELEZO)
………………………………………………………………………………………………………………………
Na Nyakongo Manyama –MAELEZO-Dar es salaam
Serikali imefanikiwa kukusanya
zaidi ya shilingi trilioni moja kwa mwezi huu tofauti na zilizokuwa
zikukusanya hapo awali za bilioni 850 kwa kipindi cha mwezi mmoja na
kuzielekeza fedha hizo kwenye miradi mbalimbali ya maendeleo.
Takwimu hizo zimetolewa leo
jijini Dar es salaam na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Dkt.
Servacius Likwelile wakati akitoa taarifa ya hali ya mapato kwa kipindi
cha mwezi Februari mwaka huu.
Amesema kuwa kati ya fedha hizo
,sekta ya elimu imepewa shilingi bilioni 18.7 kwa ajili ya utekelezaji
wa utoaji wa elimu bure kwa wanafunzi wa shule za awali hadi kidato cha
Nne ambapo fedha hizo ni kwa ajili ya malipo ya ada,chakula pamoja na
ruzuku.
Katibu Mkuu huyo ameongeza kuwa
Mkoa wa Dar es salaam imeongezewa shilingi bilioni 2 ili kupanua uwezo
wa udahili kama Rais alivyoahidi katika mkutano wake na Wazee wa Mkoa
huo.
Aidha, Dkt. Likwelile amesema
kuwa ili kuwajengea uwezo walimu walio masomoni na wakufunzi wao
,Wizara imetoa shilingi Bilioni 1.65 kwa ajili ya mafunzo kwa vitendo.
Kati ya fedha hizo wakufunzi
wamepatiwa shilingi milioni 431.6 walimu walio masomoni wametengewa
shilingi milioni 249.2 kwa ajili ya vifaa vya kufundishia, posho na
nauli.
Ameongeza kuwa fedha nyingine
kati ya hizo kiasi cha shilingi bilioni 573.7 zimetolewa kwa ajili ya
mishahara ya watumishi wa Umma , ulipaji wa deni la taifa kwa mwezi
huu zimetolewa shilingi bilioni 842.1 na Mifuko ya hifadhi za Jamii
zimetolewa shilingi bilioni 81.13.
Fedha kwa ajili ya shughlui
mbalimbali za maendeleo zimetolewa kiasi cha Shilingi Bilioni 166.2
ambapo chuo kipya cha Sayansi kilicho katika hatua ya ujenzi cha
Mlunganzi la kimepatiwa Shilingi Bilioni 18 na Kiasi cha Shilingi
Bilioni 13.6 kwa ajili ya mikopo kwa wanafunzi wa Elimu ya juu.
Mamlaka ya Elimu (TEA) imepatiwa
shilingi Bilioni 23.078, Mpango wa Maji vijijini Bilioni l7.1, maendeleo
ya ujenzi wa barabara zimetolewa shilingi bilioni 58.8, miradi ya umeme
vijijini zimetengwa shilingi bilioni 20.2, Reli shilingi bilioni
2.034, Serikali za mitaa zimepatiwa shilingi bilioni 4.5, na Mahakama
zimepatiwa shilingi bilioni 12.3.
Naye Kamishna wa Mamlaka ya
Mapato Tanzania (TRA), Alphayo Kidata amesema kuwa makusanyo yameongeza
kutoka shilingi trilioni 1.2 kwa mwezi Disemba hadi kufikia trilioni
1.79 kwa mwezi Januari
EmoticonEmoticon