Michuano ya Kombe la Shirikisho (Azam Sports Federation Cup)
inatarajiwa kuendelea wiki hii mzunguko wa nne katika hatua ya 16 bora,
kwa michezo nane kuchezwa katika viwanja mbalimbali nchini.
Jumatano Februari 24, 2016 kutakua na mchezo mmoja tu, ambapo timu ya
Young Africans watawakaribisha maafande wa JKT Mlale kutoka mkoani
Ruvuma katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam, mchezo utakaochezwa
majira ya saa 10:30 jioni.
Michezo miwili itachezwa siku ya Ijumaa ambapo, Ndanda FC watakua
wenyeji wa JKT Ruvu katika uwanja wa Nagwanda Sijaon mjini Mtwara, huku
Coastal Union wakiwakaribisha wakata miwa wa Mtibwa Sugar katika uwanja
wa Mkwakwani jijini Tanga.
Jumamosi Februari 27, Mwadui FC watawakaribisha maafande wa Rhino
Rangers katika uwanja wa Mwadui Complex mjini Shinyanga, wakati jijini
Mbeya Tanzania Prisons watacheza dhidi ya Mbeya City katika uwanja wa
Sokoine jijini humo.
Mzunguko huo wa nne utakamilika siku ya Jumapili ambapo, Simba SC
watawakaribisha Singida United katika uwanja wa Taifa jijini Dar es
salaam, Panone FC dhidi ya Azam FC uwanja wa Ushirika mjini Moshi, huku
Toto Africans wakicheza dhidi ya Geita Gold katika uwanja wa CCM Kirumba
jijini Mwanza.
NB: Rais wa TFF, Jamal Malinzi kesho Jumanne saa 5 kamili asubuhi,
ataongea na waandishi wa habari katika Ukumbi wa mikutano wa TFF uliopo
Karume.
EmoticonEmoticon