AMUUA MKE WAKE KISHA YEYE KUJINYONGA MBOZI MBEYA

December 17, 2015
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Ahmed Msangi.

Na Mwandishi wetu,Mbeya,Jamiimojablog
Katika hali isiyokuwa ya kawaida mwanaume mmoja Mkazi wa kijiji cha Malolo Ndugu  Chipunguli Mkisi (30) amemuua mke wake kwa kumkata panga kichwani kisha yeye mwenyewe kujiua kwa kujinyonga.


 Akizungumzia tukio hilo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Ndugu Ahmed Msangi amesema tukio hilo la aina yake limetokea Desemba  15 mwaka huu majira ya saa 7 mchana  huko katika kijiji cha Malolo, Kata ya Msia, wilaya ya Mbozi, Mkoa wa Mbeya.

Msangi amemtaja mwanamke huyo kuwa ni  Neva Mwaweza (24) Mkazi wa Malolo ambaye ameuwawa na mumewe kwa kukatwa  panga  kichwani . 

Kamanda Msangi amesema chanzo cha tukio hilo  ni wivu wa kimapenzi baada ya mwanaume kumtuhumu mke wake kuwa na mahusiano ya kimapenzi na mwanaume mwingine.

inadaiwa kuwa baada ya tukio, mtuhumiwa alijinyonga kwa kutumia kamba kwenye mti umbali wa mita 100 kutoka nyumbani kwake.

Aidha mwili wa marehemu [mwanaume] ulikutwa ukiwa na majeraha kwenye vidole na kando kukiwa na panga na alikutwa na ujumbe uliokuwa na maneno “kuwa ameamua kumuua mke wake na yeye kujinyonga kutokana na mke wake kuwa na mahusiana ya kimapenzi na mwanaume mwingine aitwae kilasi nzowa

Miili ya marehemu imehifadhiwa katika hospitali ya wilaya vwawa. ambapo kwa mujibu Kamanda Msangi uchunguzi wa tukio hilo  unaendelea.
Mwisho.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »