Baadhi ya wahitimu wakijiaandaa
kabla ya kuanza maandamano kuelekea eneo la kutunuku vyeti wakati wa
mahafali ya 37 yaliyofanyika katika kituo cha NBAA Mbweni jana jijini
Dar es Salaam.
Bendi ya Jeshi la Kujenga Taifa
(JKT) wakiongoza maandamano kuelekea eneo la kutunuku vyeti wakati wa
mahafali ya 37 yaliyofanyika katika kituo cha NBAA Mbweni jana jijini
Dar es Salaam.
Mgeni rasmi ambaye pia ni Waziri
wa Nchi Ofisi ya Rais (Kazi Maalum), Prof. Mark Mwandosya akiongea na
wahitimu wakati wa mahafali ya 37 ya Bodi ya Taifa na Wakaguzi wa Hesabu
nchini (NBAA) na wageni waalikwa yaliyofanyika jana katika kituo cha
NBAA Mbweni jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Bodi ya Taifa na
Wakaguzi wa Hesabu nchini (NBAA) Prof. Isaya Jairo akimkaribisha Mgeni
rasmi ambaye pia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Kazi Maalum), Prof.
Mark Mwandosya kuongea na wahitimu wakati wa mahafali ya 37 wa Bodi hiyo
pamoja na wageni waalikwa yaliyofanyika jana katika kituo cha NBAA
Mbweni jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Bodi ya Taifa na
Wakaguzi wa Hesabu nchini (NBAA) Bw. Pius Maneno akitoa hotuba fupi kwa
mgeni rasmi wakati wa mahafali ya 37 yaliyofanyika katika kituo cha NBAA
Mbweni jana jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wahitimu wa Bodi NBAA
wakifuatilia kwa makini hotuba ya Mgeni rasmi wakati wa mahafali ya 37
yaliyofanyika katika kituo cha NBAA Mbweni jana jijini Dar es Salaam
ambapo jumla ya wahitimu 972 walipata CPA na wahitimu 87 walipata cheti
cha utunzaji wa hesabu.
Mgeni rasmi ambaye pia ni Waziri
wa Nchi Ofisi ya Rais (Kazi Maalum), Prof. Mark Mwandosya akimpongeza
mmoja wa wahitimu wa CPA aliyefanya vizuri kwenye mitihani yake wakati
wa mahafali ya 37 yaliyofanyika katika kituo cha NBAA Mbweni jana jijini
Dar es Salaam.
Mgeni rasmi ambaye pia ni Waziri
wa Nchi Ofisi ya Rais (Kazi Maalum), Prof. Mark Mwandosya akiwa katika
picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa Bodi ya Taifa na Wakaguzi wa
Hesabu nchini (NBAA) na wahitimu CPA wakati wa mahafali ya 37
yaliyofanyika jana katika kituo cha NBAA Mbweni jijini Dar es Salaam.
..……………………………………………………………………….
Na Eleuteri Mangi-MAELEZO
Wahitimu wa Bodi ya Taifa na
Wakaguzi wa Hesabu nchini (NBAA) ambao ni wataalamu wa masuala ya
uhasibu na ukaguzi wa hesabu wameaswa kulinda, kutunza na kusimamia
viapo vyao wakati wakitekeleza majukumu yao ya kihasibu ipasavyo katika
sehemu zao za kazi
Hayo yamesemwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Kazi Maalum),
Prof. Mark Mwandosya wakati wa mahafali ya 37 ya Bodi ya NBAA
yaliyofanyika jana katika kituo cha NBAA Mbweni jijini Dar es Salaam.
“Kiapo mlichoapa leo kiwe chachu ya ufanisi katika utendaji wenu
wa kazi, kushuka kwa kiwango cha maadili katika utumishi kunatokana na
kuota kwa mizizi katika suala la fedha”
Prof. Mwandosya aliendelea kusisitiza, “Mlinzi mkuu wa fedha
katika sehemu yeyote ile ni Mhasibu, nanyi leo mnahitimu, mnapaswa kuwa
waaminifu kwa familia zenu, taaluma yenu na kwa taifa mkiongozwa na
kiapo mlichoapa, isiwe ni sehemu ya ajenda ya leo ya kutimiza wajibu,
bali kiapo hicho kiwe cha kusisitiza maadili, uaminifu, uadilifu na
uzalendo”.
Aidha, Prof. Mwandosya aliongeza kuwa Bodi ya NBAA na Watanzania
wana wajibu wa kujenga fikra ya kizalendo kwa taifa lao na kujiamini
katika masuala ya hesabu za fedha ili waweze kufikia viwango vya
kimataifa kwa kuweka misingi imara kwa wahasibu na wakaguzi wa hesabu
ambapo mataifa mengine wavutiwe kuja kujifunza hapa nchini.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Mtendaji Bodi ya Taifa na Wakaguzi
wa Hesabu Tanzania (NBAA) Bw. Pius Maneno akitoa taarifa ya Bodi hiyo
kwa mgeni rasmi wakati wa maafali hayo alisema kuwa kituo hicho
kimefanikiwa kinatoa mchango mkubwa nchi katika kukuza fani ya wahasibu
na wakaguzi wa hesabu nchini tofauti na hali ilivyokuwa miaka ya nyuma.
Katika mahafali hayo, idadi ya wahitimu imeongezeka mwaka huu na
kufikia 972 waliopata CPA na wahitimu 87 kwa ngazi ya cheti cha
utunzaji wa hesabu tofauti na hali ilivyokuwa mwaka jana 2014 ambapo
kulikuwa na jumla ya wahitimu 855 walipata CPA na wahitimu 82 walipata
cheti cha utunzaji wa hesabu.
Wakati huo huo, mmoja wa wahitimu hao Imelda Mzatulla alisema
kuwa kiapo walichoapa kinawahamasisha kutimiza wajibu wao kwa mujibu wa
kanuni za maadili ya kiuhasibu na ukaguzi wa hesabu, kwa uaminifu,
uadilifu na utaalamu kwa kuzingatia matarajio ya Serikali, muajiri,
jamii na taifa kwa ujumla.
Kiapo hicho walichoapa wahitimu hao, pia kinawahimiza kuwa
waendelee kushirikiana na kituo hicho cha NBAA kwa kuzingatia miongozo
yote ya taaluma yao inayotolewa na Bodi hiyo nchini.