Msoma
Utenzi akisoma Utenzi maalum wakati wa Uzinduzi wa Mkutano wa Kampeni wa
Jimbo la Chumbuni Unguja uliofanyika katika Viwanja vya Mabanda ya
Ngombe Chumbuni Zanzibar.
Mwanachama
wa Chama cha Mapinduzi akiwa katika viwanja vya mkutano akishangilia na
Picha ya Mgombea wake wa Ubunge kupitia CCM Ndg. Ussi Salum Pondeza
AMJADI wakati wa mkutano huo
Wananchi
wa Jimbo la Chumbuni wakiwa katika viwanja vya mkutano wa Kampeni ya
Mbunge na Mwakilishi wa Jimbo hilo uliofanyika viwanja vya Mabanda ya
Ngombe Chumbuni Unguja.
Wagombea
Ubunge Uwakilishi na Udiwani wakiwapungia mikono Wananchi waliohudhuria
mkutano huo wa kampeni wakati msoma utenzi akitaja majina ya Wagombea.
Wanachama
wa CCM wa Tawi la Masumbani Jimbo la Chumbuni wakifuatilia mkutano huo
wa kampeni uliofanyika viwanja vya mabanda ya ngombe chumbuni Unguja
Mgombea
Ubunge Jimbo la Mfenesini Kanali Mstaaf Masoud akimtunza msoma Utenzi
wakati wa mkutano wa Uzinduzi wa Jimbo la Chumbuni Unguja.
Katibu wa CCM Jimbo la Chumbuni akisoma utaratibu wa mkutano huo wa kampeni wa jimbo hilo.
Aliyekuwa
Mwakilishi wa Jimbo la Chumbuni Unguja Mhe Machano Othman, akiwasalimia
Wananchi wa Jimbo hilo na kuwaombea Kura Wagombea wote wa CCM
wanaogombea katika Jimbo la Chumbuni kuazi Mbunge Mwakilishi na Madiwani
kuwa kura ya Ndio kuendelea maendeleo katika jimbo hilo walioyawacha
wao.kwa sasa anagombea Jimbo la Mfenesini nafasi ya Uwakilishi
Mwenyekiti
wa Wazazi Mkoa wa Kusini Unguja Mhe Haji Ameir akizungua mkutano wa
Kampeni wa Jimbo la Chumbuni Unguja uliofanyika katika viwanja vya mpira
mabanda ya ngombe chumbuni na Kuwatambulisha Wagombea wa CCM wa Jimbo
hilo.na kuwaombea Kura siku ya Uchaguzi Mkuu kwa kura ya Ndio, pamoja na
Rais wa Zanzibar Dk Shein, na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania
Dk John Pombe Magufuli.
Wanachama wa CCM wakiwa katika viwanja vya Kampeni wakishangilia na Vipeperushi vya wagombea wa Jimbo la Chumbuni Unguja.
Mwenyekiti
wa Jumuiya ya Wazazi Mkoa wa Kusini Unguja Mhe Haji Ameir
akimtambulisha Mgombea Ubunge wa Jimbo la Chumbuni Ussi Salum Pondeza
AMJADI, wakati wa mkutano wa Kampeni wa Jimbo la Chumbuni uliofanyika
katika viwanja vya Mabanda ya Ngombe Chumbuni.
Mgombea
Ubunge Jimbo la Chumbuni Ussi Salum Pondeza AMJADI akiwataka Wananchi
wa Jimbo la Chumbuni kujiandaa na Maendeleo katika Jimbo hilo katika
kipindi chake cha miaka mitano kuweza kulibandilisha Jimbo hilo katika
maendeleo kwa Vijana na Wazee katika sekta mbalimbali zikiwemo za Elimu,
Maji, Kujiajiri Wenyewe na Afya. amewataka kumpigia Kura ya Ndio kuweza
kuwaletea maendeleo hayo.
Mgombea
Ubunge wa Jimbo la Chumbuni akimwaga Serazake kwa Wananchi wa Jimbo la
Chumbuni wakati wa mkutano wake wa kampeni katika viwanja vya mpira
mabanda ya ngombe chumbuni Unguja.
Wanachama wa CCM wakishangilia wakati wa mkutano wa kampeni wa Jimbo la Chumbuni Unguja
Wanachama
wa CCM wakishangilia wakati wa mkutano wa kampeni wa Jimbo la Chumbuni
Unguja wakati akihutubia Mgombea Ubunge wa Jimbo hilo Ussi Salum Pondeza
AMJADI, uliofanyika viwanja vya mabanda ya ngombe chumbuni Unguja.
Wananchi wa Jimbo la Chumbuni wakifuatilia Mkutano wa Kampeni wa Jimbo hilo uliofanyika viwanja vya mabanda ya ngombe chumbuni.
Mgombea
Uwakilishi wa Jimbo la Chumbuni Miraj Kwaza akiwahutubia Wananchi wa
Jimbo la Chumbuni Unguja wakati wa mkutano wa kampeni wa Jimbo hilo na
kusoma baadhi ya vipengele vya Ilani ya Uchaguzi ya CCM jinsi
itakavyotekelezwa katika kipindi cha miaka mitano ijayo ya Dk Shein.
Wanachama wa CCM wakishangilia wakati wa mkutano huo wa Kampeni ya Jimbo la Chumbuni Unguja
Msanii
wa Bendi ya Yamoto, akitowa burudani kwa Wanachama wa CCM wa Jimbo la
Chumbuni wakati wa Mkutano wa Kampeni wa Jimbo hilo.
Wanachama wa CCM wakishangilia wakati wa mkutano huo wa Kampeni ya Jimbo la Chumbuni Unguja
Mwenyekiti
wa Jumuiya ya Wazazi Mkoa wa Kusini Unguja Mhe Haji Ameir,
akimtambulisha Mgombea Udiwani wa Wadi ya Chumbuni, Ndg. Mussa Haji
Idrisa kwa Wananchi wa Jimbo hilo
Mgombea Udiwani Wadi ya Chumbuni Ndg Mussa Haji Idrisa. akiwasalimia Wananchi wakati akitambulishwa na kuomba Kura.
Mgombea Udiwani Wadi ya MuembemakundiNdg Haji Juma, akiwasalimia Wananchi wakati akitambulishwa na kuomba Kura.
Mgombea Udiwani Wadi ya MuembemakundiNdg.Haji Juma. akiwasalimia Wananchi wakati akitambulishwa na kuomba Kura.
Imetayarisha na OthmanMapara.Blogspo. Zanzinews.com
Email othmanmaulid@gmail.com
Mobile. 0777424152 or 0715424152