KWA USHIRIKIANO NA HALMSHAURI YA JIJI GENERETA YA HOSPTALI ITAPATIKANA.

October 05, 2015


Wakazi wa Kata ya Pongwe wakimsikiliza Mgombea Udiwani wa CCM,Bw.Mbaraka Saad Mbaraka akinadi sera zake.     

Mgombea Udiwani  Kata ya Marungu(CCM)Bw.Mohamed Mambeya(kulia) akimnadi Mgombea Udiwani kata ya Pongwe Mbaraka Saad Mbaraka wakati wa kampeni eneo la Kifumbi Pongwe.
Mohamed Mambeya akipanda Jukwaani kumnadi Mgombea Udiwani kata ya Pongwe Mbaraka Saad.
 Wakazi wa Pongwe wakimsikiliza Mohamed Mambeya wakati wa Kampeni ya Mbaraka Saad Mbaraka Kifumbi,Pongwe.




 Mbaraka Saad Mbaraka akisifiwa na mwana CCM aliyejitokeza kwenye kampeni yake Pongwe.

 Mgombea Udiwani CCM kata ya Pongwe Mbaraka Saad Mbaraka akizungumza na Wananchi wa kata hiyo wakati wa mkutano wa kampeni.
Baadhi ya Viongozi wa Chama waliokuwepo kwenye mkutano.

Mgombea Udiwani kupitia CCM katika kata ya Pongwe Mbaraka Saad Mbaraka amesema endapo atachaguliwa kuwa Diwani wa Kata hiyo na kuwatumikia wananchi atahakikisha kuwa Zahanati iliyopo kwenye kata hiyo inapata Genereta.

Akizungumza wakati wa Kampeni yake iliyofanyika eneo la Kifumbi Pongwe,amesema atahakikisha anashirikiana na Halmashauri ili kufanikisha hilo.

Amesema watumiaji wa Zahanati hiyo wanapata tabu kwa kuwa imekuwa kubwa ambayo inafanyia watu upasuaji wa aina mbalimbali na kutokana na umeme kukatika inawafanya wanachi kuwa katika hali ya hatari pindi anapokua kwenye upasuaji.

Hata hivyo ameongeza kuwa vijana watafaidika na asilimia kumi inayotolewa na Halmashauri ili waweze kujiendeleza kwa kujikopesha.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »