Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF) limepokea maombi ya klabu
ya Young Africans (Yanga SC) ya kutaka kufanya uchaguzi wake mkuu wa
viongozi wa klabu hiyo kwa nafasi za Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti na
wajumbe wa kamati ya Utendaji.
TFF imeiomba klabu hiyo kufanya mkutano wake wa Uchaguzi wa viongozi
baada ya kufanyika kwa Uchaguzi Mkuu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania (Rais, Wabunge na Madiwani) utakaofanyika Oktoba 25, 2015.
Hii ni kutokana na unyeti wa uchaguzi wa klabu ya Yanga yenye matawi nchini kote.