Kampuni ya mawasiliano ya Vodacom Tanzania, ambayo ni mdhamini mkuu
wa Ligi Kuu ya mpira wa miguu Tanzania bara leo imekabbidhi vifaa kwa
timu zinazoshiriki ligi hiyo yenye thamani ya shilingi milioni
490,00,000.
Akikabidhi vifaa hivyo leo jijini Dar es salaam, Mkuu wa Kitengo cha
Masoko na Mawasiliano wa Vodacom Kelvin Twisa alsiema kuwa kwa mara
nyingine tena katika kuhakikisha ligi ya soka nchini inaenda vizuri
Vodacom inakidhi vifaa mbalimbali vy a ligi ambavyo ni jezi za kawaida,
jezi za mechi, viatu na vifaa vingine vinayohitajika.
“Tunajisikia furaha kukabidhi vifaa hivi siku ya leo tukiwaa
tunatekeleza matakwa ya mkataba wa udhamini, ni imani yetu kwamba timu
zitakazoshiriki lii zimejiandaa vya kutosha kwa msimu mpya 2015/2016”
Alisema Twissa.
Twissa alisema Vodacom inaendelea kudhamini ligi kuu kwa sababu soka
ni mchezo unaopendwa sana hapa nyumbani ukiwa na washabiki wengi hivyo
inapenda kuona wananchi ambao baadhi yao ni wateja wake wanapata
buruddaniya mchezo waupendao pia siku zote inaamini kuwa michezo ni
ajira kubwa duniani kote, ikiendelezwa inaweza kubadilisha maisha ya
watu wengi na taifa kunufaika kwa mapato makubwa ya kodi kutoka sekta
hii.
Aliwataka wadhamini wengine kujitokeza ili kuboresha zaidi ligi ya
Tanzania na kuongeza maslahi kwa wachezaji wanaoshiri katika ligi
“Tukiunganisha nguvu timu zetu zinaweza kuwa na wachezaji wa kimataifa
pia ni muhimu kwa wadau mbalimbali kuanza kuwekeza katika timu za vijana
chipukizi kwa kuwa vipaji vinaanza ngazi ya chini ambako vinapaswa
kuibuliwa na kuendelezwa” Alisema Twissa.
Naye Ofisa Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi, Boniface Wambura
aliishukuru Kampuni ya Vodacom na kuvitaka vilabu vinavyoshiriki ligi
kuu ya Vodacom kuheshimu chapa ya mdhamini wakati wote wa ligi.
“Ninatoa mwito kwa vilabu vyote kutumia jezi zenye nembo ya mdhamini
katika kuhakikisha ligi inafanikiwa kama inavyotakiwa” alisema.
Aliongeza kuwa TFF isingependa kutumia kanuni na sharia kuadhibu
klabu inayokwenda kinyume, bali kila klabu izingatie masharti ya
madhamini kama ambavyo anavyotimiza haki yake ya kuwapatia vifaa.
Alisema ligi ya mwaka huu itakuwa bora kutokana na maandalizi yote
kukamilika mapema pia timu zitakazoshiriki zimejiandaa vya kutosha
kuhakikisha ligi inakuwa na msisimko na ushindani mkubwa.