Wachimbaji madini wadogo waipongeza Serikali

August 20, 2015

 Mwenyekiti wa Shirikisho la Vyama vya Wachimbaji Madini Tanzania (FEMATA), Gregory Kibusi akiwasilisha mada kuhusu wachimbaji wadogo wa madini katika Semina ya Wathamini Madini ya Vito na Almasi nchini, iliyofanyika hivi karibuni (Agosti 12 na 13, 2015) katika Hoteli ya Gold Crest jijini Mwanza.
 Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimaliwatu, Mrimia Mchomvu, akitoa hotuba ya kufunga Semina ya Wathamini Madini ya Vito na Almasi nchini iliyofanyika hivi karibuni (Agosti 12 na 13, 2015) katika Hoteli ya Gold Crest jijini Mwanza.
 Baadhi ya washiriki wa Semina ya Wathamini Madini ya Vito na Almasi nchini, wakifuatilia kwa umakini mada zilizokuwa zikiwasilishwa. Semina hiyo ilifanyika hivi karibuni (Agosti 12 na 13, 2015) katika Hoteli ya Gold Crest jijini Mwanza.
 Mkurugenzi wa Kitengo cha Uthaminishaji wa Madini ya Almasi na Vito cha Wizara ya Nishati na Madini (TANSORT), Archard Kalugendo, akiwasilisha mada kuhusu majukumu ya Kitengo hicho katika Semina ya Wathamini Madini ya Vito na Almasi nchini iliyofanyika hivi karibuni (Agosti 12 na 13, 2015) katika Hoteli ya Gold Crest jijini Mwanza.
 Baadhi ya washiriki wa Semina ya Wathamini Madini ya Vito na Almasi nchini, wakifuatilia kwa umakini mada zilizokuwa zikiwasilishwa. Semina hiyo ilifanyika hivi karibuni (Agosti 12 na 13, 2015) katika Hoteli ya Gold Crest jijini Mwanza.
 Afisa kutoka Kitengo cha Uthaminishaji wa Madini ya Almasi na Vito cha Wizara ya Nishati na Madini (TANSORT), Salome Tilumanywa, akiwasilisha mada kuhusu uchimbaji na biashara ya tanzanite katika Semina ya Wathamini Madini ya Vito na Almasi nchini, iliyofanyika hivi karibuni (Agosti 12 na 13, 2015) katika Hoteli ya Gold Crest jijini Mwanza.
Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Ngosi Mwihava (Wa pili kushoto – waliokaa mbele), akiwa katika picha ya pamoja na Washiriki wa Semina ya Wathamini Madini ya Vito na Almasi. Wengine kutoka Kulia (waliokaa) ni Kamishna Msaidizi wa Madini Kanda ya Ziwa Victoria - Magharibi, Mhandisi David Mulabwa, Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimaliwatu Mrimia Mchomvu, pamoja na Mkurugenzi wa Kitengo cha Uthaminishaji wa Madini ya Almasi na Vito cha Wizara ya Nishati na Madini (TANSORT), Archard Kalugendo.
Wachimbaji madini wadogo waipongeza Serikali
Na Veronica Simba – aliyekuwa Mwanza
Shirikisho la Vyama vya Wachimbaji Madini Tanzania (FEMATA), limetoa pongezi kwa Serikali kupitia Wizara ya Nishati na Madini, hususani Kitengo cha Uthaminishaji Madini ya Vito na Almasi (TANSORT), kwa jitihada inazofanya kuwainua wachimbaji wadogo nchini.
Pongezi hizo zilitolewa hivi karibuni na Mwenyekiti wa FEMATA, Gregory Kibusi wakati akiwasilisha mada kuhusu wachimbaji wadogo wa madini katika Semina ya Wathaminishaji Madini ya Vito na Almasi iliyofanyika Agosti 12 na 13, Hoteli ya Gold Crest jijini Mwanza.
“Kwa niaba ya uongozi wa FEMATA, naipongeza Serikali hasa Kitengo cha TANSORT kupitia Wizara ya Nishati na Madini, kwa jitihada za makusudi kabisa za kuwainua wachimbaji wadogo nchini.” 
Akifafanua zaidi, Kibusi alisema kuwa wachimbaji wadogo wamekuwa wakikutana na changamoto nyingi lakini kutokana na ushirikiano ambao Serikali inautoa, hakuna shaka malengo yaliyomo katika Sera ya Madini ya Mwaka 2009 yatatimia.

Kibusi alisema, kupitia jitihada zinazofanywa na Serikali, wachimbaji wadogo wamekuwa na mwamko wa kupata taarifa za mipango na mikakati ya Serikali juu ya maendeleo yao.Pia, alisema jitihada za Serikali zimewezesha wachimbaji wadogo kushiriki maonesho ya madini ya vito na usonara ya ndani na nje ya nchi. 
“Aidha, Serikali kupitia Wizara ya Nishati na Madini imeanza kutoa ruzuku kwa wachimbaji wadogo sambamba na Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) kuwa mlezi wa wachimbaji wao,” alisema Kibusi.
Kibusi alisema wachimbaji wadogo wanakumbana na changamoto kadhaa ikiwa ni pamoja na uwezo mdogo wa kifedha katika kuendesha shughuli zao za uchimbaji na ukosefu wa elimu ya juu ya madini hasa ya vito.
Alitaja changamoto nyingine kuwa ni wachimbaji wadogo wa madini kutotambuliwa na baadhi ya Taasisi za Serikali na zisizo za kiserikali kama wadau wakubwa wa maendeleo hasa kiuchumi na kijamii.
Akiwasilisha maombi ya FEMATA kwa Serikali, Kibusi alisema wachimbaji wadogo wanahitaji wataalamu wa madini ya vito ili wawasaidie katika masuala mbalimbali ikiwa ni pamoja na kutambua, kuthamini, kusaidia kutafuta masoko pamoja na kutoa ushauri juu ya uongezaji thamani madini na namna bora ya kufanya biashara ya madini. 

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »