Mshindi
wa Shindano lala Mama Shujaa wa Chakula Msimu wa Nne mwaka 2015
Calorina Chilele Muda mchache Baada ya kutangazwa kuwa mshindi.
Afisa
Kilimo Mkuu Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika Dkt. Kissa Kajigili ,
akiwapongeza Oxfam kwa kuandaa shindano la Mama Shujaa wa Chakula na
washiriki wote kwa ujumla walioshiriki katika Shindano hilo, Pia
alimpongeza Mshindi wa Mama Shujaa wa Chakula 2015 Carolina Chilele na
kumtaka awe mfano bora pia akawe chachu ya kuinua kilimo na kuwasaidia
wenye uhitaji yaani wakulima wanawake wadogo wadogo, Mwisho aliwaomba
Oxfam waendelee na Shindano hili muhimu.
Jackson Yusuph Mzumba Mwenyekiti wa Kitongoji cha Kibweni akitoa neno la Shukurani kwa niaba ya Serikali ya Kijiji cha Kisanga
Kaimu
Mkurugenzi Mtendaji Wilaya ya Kisarawe Bw. Ellioth Phillemon
Mwasambwite akiwashukuru Washiriki wa Shindano la Mama Shujaa wa Chakula
2015 , na kuwaaaga rasmi, pia kumpongeza Mshindi wa Shindano hilo msimu
wa Nne Bi. Carolina Chilele , Mwisho aliwapongeza Oxfam kwa kuanzisha
shindano endelevu kwa Maendeleo ya wakulima hasa wanawake.
Mmoja
wa akina mama ambao walikuwa wanakaa na Washiriki wa Shindano la Mama
Shujaa wa Chakula katika Kijiji cha Kisanga Bi. Sophia Shomvi akitoa
neno la Shukurani kwa washiriki hao kwa jinsi walivyo kaa vizuri pamoja
na pia kuwaachia elimu kubwa wanakijiji hao. Mwisho alitoa neno la
Kuwaaga Rasmi